728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, October 15, 2016

  Shule ya ATLAS yafanya Mahafali ya Darasa la Saba, Wazazi na Walezi Watakiwa kutowakatishaTamaa Watoto  Shule ya Atlas Madale iliyopo Jijini Dar es Salaam imefanya mahafali ya Darasa la saba, ambapo Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo alikuwa ni ndugu Rogers Shemwelekwa, ambae ni Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni.  Mkuu wa Shule ya Atlas Madale Justus Kagya akizungumza katika Mahafali hayo ameeleza kuwa kila mwaka ifikapo Oktoba 14 shule hiyo imejiwekea utaratibu wa kufanya mahafali ili Kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu JULIUS NYERERE.  Makamu mkuu upande wa Taaluma kwenye shule hiyo Joseph Mjingo amewataka Wazazi kuacha kuwakatisha tamaa Watoto, hususani kwenye Somo la Hesabu, ambalo limekuwa likionekana kuwa ni gumu tofauti na masomo mengine

  Aidha Mahafali hayo yamehudhuriwa na Wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi hao.

  Afisa Elimu wa manispaa ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa akizungumza na Wahitimu wanaomaliza Darasa la Saba katika Shule ya Atlas madale iliyopo Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Shule ya Atlas madale, Justus Kagya akitoa nasaha zake kwa wahitimu wanaomaliza Darasa la Saba, wakati wa Mahafali yaliyofanyika kwenye Shule hiyo, ambapo Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni ndugu Rogers Shemwelekwa.
  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakipata maelezo ya kina kutoka kwa mkuu wa Shule ya Atlas madale, ndugu Justus Kagya wakati wa mahafali ya wahitimu wa Darasa la saba kwenye shule, ambayo pia yalihudhuriwa na wazazi na walezi wa wanafunzi hao.
  Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi katika Shule ya Atlas madale ya Jijini Da es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye Shughuli hiyo.
  Baadhi ya Wahitimu wanaomaliza elimu ya msingi katika shule ya Atlas madale wakionesha nyuso za furaha, baada ya kusikia nasaha kutoka kwa Afisa elimu wa manispaa ya Kinondoni ndugu Rogers Shemwelekwa pamoja na mkuu wa shule hiyo ndugu Justus Kagya. 
  Sehemu ya Wanafunzi wa Atlas madale waliohudhuria Mahafali ya wahitimu wa Darasa la Saba kwenye Shule hiyo.
  Baadhi ya watumishi wa Shule ya Atlas Madale wakiwa wamepanda Jukwaani wakati wa mahafali ya Darasa la Saba kwenye shule hiyo, yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
  Wageni waalikwa wakiwemo Wazazi na walezi wa wanafunzi wanaohitimu elimu ya Msingi kwenye Shule ya Atlas madale, wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kupata chakula cha Mchana kilichoandaliwa maalum na uongozi wa shule hiyo.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Shule ya ATLAS yafanya Mahafali ya Darasa la Saba, Wazazi na Walezi Watakiwa kutowakatishaTamaa Watoto Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top