728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, October 29, 2016

  SHIWATA yandaa mashindano

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)umeandaa mashindano ya Sanaa na Michezo litakalofanyika kuanzia Novemba 12,2016 katika viwanja
  mbalimbali jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema jana kuwa michezo
  itakayoshindaniwa ni soka,mpira wa kikapu,ngoma za asili, muziki wa
  dansi, sarakasi, Karate na kaswida.

  Alisema mashindano hayo yatafanyika kuwapata washindi ambao kwa pamoja watakwenda kukabidhiwa zawadi zao kwenye kijiji cha wasanii
  Mwanzega,Mkuranga.

  Mwenyekiti Taalib aliwataja wajumbe wa Kamati ya tamasha hilo kuwa ni
  Deo Kway, na mchezaji wa zamani wa Simba, Kureshi Ufunguo na mchezaji
  wa zamani wa Yanga, Salvatory Edward watakaosimamia mashindano ya
  soka.

  Wengine ni Selemani Pembe, Athumani Bakari maarufu kama Mbegeja katika mchezo wa sarakasi,Abdul Salvador kamati ya muziki wa dansi na Kocha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu, Manase Zablon katika mchezo wa mpira wa kikapu.

  Wajumbe wengine ni Ismail Kambangwa, Kashindye Fundikira na Mariam
  Ismail maarufu kama mama Mipango watakaosimamia ngoma za asili.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SHIWATA yandaa mashindano Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top