728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, October 6, 2016

  SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LATANUA WIGO WAKE AFRIKA KUPITIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA KULULA.COM

  SHIRIKA la Ndege la Etihad lenye makao makuu yake Nchi za Falme za Kiarabu limeendelea kujihimarisha barani Afrika kupitia ushirikianao mpya wa kibiashara walioingia na Kulula, washindi wa tuzo ya ndege ya gharama nafuu nchini Afrika Kusini.

  Ushirikiano huo wa biashara utawawezesha wateja wa Shirika la Ndege la Etihad kufika miji mbalimbali ndani ya Afrika Kusini ikiwamo miji ya Cape Town, Durban, George na East London via Johannesburg.

  Shirika la Ndege la Etihad litaweka namba yake ya EY kwenye ratiba za ndege za Kulula kati ya Johannesburg na miji mingine mikubwa maarufu. Makubaliano hayo yanamwezesha mteja kupatiwa huduma zote anapoanza safari na anakofikia.

  Huduma hiyo mpya itaanza kuuzwa kuanzia Octoba 3, 2016 kwa kuanza na safari kutoka maeneo ya Kaskazini kwa ratiba ya tarehe 30 Octoba mwaka huu.

  Makubaliano hayo baina ya Shirika la Ndege la Etihad na Kulula ni mwendelezo wa juhudi za shirika hilo kutokana na dhamira yake ya kuongeza idadi ya safari za ndege zake zinazotoa huduma kwenye bara hili kwenye maeneo 23 kupitia ushirikiano uliopo kupitia Shirika la Kenya Airways, Royal Air Maroc na mpango wa ushirikiano ulipo kwenye Shirika la Air Seychelles.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Peter Baumgarter alisema, “Shirika la Ndege la Kulula limekuwa na ubunifu wa hali ya juu na mshindi wa tuzo ya usafiri wa anga hivyo makubaliano haya ya kibiashara kwenye sekta ya anga yanadhihirisha juhudi za Shirika la Ndege la Etihad katika kupanua shughuli zake za kibiashara barani Afrika. Kupitia mkataba huu Kulula itawapa huduma wateja wetu wanaotoka Johannesburg kupitia safari nne zilizoanzishwa katika ukanda huo. Ni matumaini yangu ushirikiano huu ulioanzishwa utaleta manufaa kwa wasafiri wa daraja la biashara na wale wa starehe kwa usawa.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya mama Comair ya Kulula, Erik Vanter alisema,
  “Tunajivunia kushirikiana na Shirika la ndege la etihad kuwa miongoni wa washirika wetu kwenye huduma za usafiri wa anga na kuwa chachu kwenye kuongeza fursa za ushirikiano. Tunawakaribisha wateja wa Shirika la Ndege la Etihad kwa moyo mkunjufu kwenye jumuiya yetu ya usafirishaji.

  Kwa barani Afrika Shirika hilo la ndege la Etihad linatoa huduma zake kwenye miji 10 barani afrika ambayo ni Johannesburg, Nairobi, Entebbe, Dar es Salaam, Khartoum, Casablanca, Rabat, Lagos, Cairo na Mahé visiwa vya Seychelles.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LATANUA WIGO WAKE AFRIKA KUPITIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA KULULA.COM Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top