728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, October 5, 2016

  SERIKALI KUANDAA MTAALA KWA WATUMISHI WA MAJUMBANI KATIKA NCHI ZA MASHARIKI YA KATI

  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

  Serikali inaandaa mtaala wa kuongeza ustadi na ujuzi kwa watanzania  wanaofanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati.

  Hayo yamebainishwa  leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima alipokuwa akikanusha habari iliyotolewa na Gazeti la Tanzania Mpya la Oktoba 04,Mwaka huu,Toleo namba 23 katika Ukurasa wa 4, lililokuwa na habari iliyosema “Watanzania wateswa nchini Oman na wengine hunyofolewa figo zao na kupewa ndugu wa  waajiri wenye mahitaji”.

  Kutokana na hayo Balozi Kilima  alifafanua kuwa habari hiyo haina ukweli wowote,isipokuwa ni maoni binafsi ya mwandishi  wa  gazeti hilo na hayawakilishi msimamo wa Serikali kuhusu masula ya wafanyakazi za ndani wakitanzania nchini Omani.

  Aidha, Balozi huyo amesisitiza kuwa nia ya Serikali ya kuanzisha mtaala huo ni katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba nazo watanzania wanaofanyakazi za ndani nchini Oman.

  “Serikali imeazimia kutumia Chuo cha Ufundi Stadi (VETA)  ili kutoa mtaala utakaosaidia kutoa mafunzo kwa maana ya utaratibu na utamaduni wa nchi wanazokwenda kufanyakazi, ili kusaidia  watanzania kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu kazi husika na changamoto zake kabla ya kukubali kufanyakazi hizo,” alisema Balozi Kilima

  Sambamba na hilo Serikali imeendelea kuwataka watanzania kufuata utaratibu kabla ya kwenda kufanyakazi katika nchi hizo kwa kutumia mawakala rasmi wa ajira walioandikishwa na mamlaka husika pamoja na kuwepo mkataba wa ajira unaotambuliwa na Mamlaka za nchi wanazookwenda  ili kuepuka usumbufu na changamoto wanazoweza kuzipata ikiwemo kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili.

  Balozi Mwilima ameongoza kuwa  katika kupata suluhisho la kudumu  katika  kuwasaidia watanzania kupata fursa za ajira nje ya nchi,Wizara kwa kushiririkiana na wadau  imeendelea kufanya jitihada  za kusaini Mikataba ya Ushirikiano katika Sekta ya ajira na kazi baina ya Serikali ya Tanzania na nchi mbalimbali.

  Watanzania  5600 wanakadiriwa  kufanyakazi katika kada za madaktari, walimu, wauguzi, wahadhiri, wapishi, wahudumu wa mashambani na bustani na watumishi wa nyumbani, na kati ya hao karibu watanzania 200 ndio wanaofanyakazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SERIKALI KUANDAA MTAALA KWA WATUMISHI WA MAJUMBANI KATIKA NCHI ZA MASHARIKI YA KATI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top