728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, October 11, 2016

  Serikali imeunda kikosi kazi kutafuta ufumbuzi wa kudumu katika kutatua changamoto sekta ya ardhi

  NA Beatrice Lyimo-MAELEZO
  Dar es Salaam.

  Serikali imeunda kikosi kazi chenye wajumbe kutoka wizara sita zinazoshukulika na masuala ya ardhi ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa kudumu katika kutatua changamoto mbali mbali za ardhi ikiwemo maeneo ya Hifadhi.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaamu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani alisema kuwa lengo la kuhusisha Wizara hizo ni kufanya uchunguzi wa kina na wa kisheria kuhusu namna bora na endelevu ya kumaliza changamoto katika sekta ya ardhi.

  “Serikali imeamua kuunda kikosi kazi chenye wajumbe kutoka Wizara ya Ardhi ikiwa ni wadau wakuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo kwa madhumuni mapana ya kufanya uchunguzi wa kina na kupitia sheria zote endelevu za kumaliza changamoto za ardhi inayohusisha maeneo ya hifadhi” alifafanua Mhandisi Kamani

  Mhandisi Makani alisema kuwa kikosi hicho kimeanza kufanya kazi ya kusoma taarifa mbalimbali za baadhi ya maeneo yenye changamoto za ardhi na hivi karibuni kinatarajia kutembelea maeneo hayo ili kujua chanzo cha matatizo na jinsi ya kushughulikia changamoto hizo.

  Aidha, katika hatua hiyo ya Serikali ya kuendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu na endelevu wa changamoto za ardhi, Mhandisi Makani amewataka viongozi na watumishi wanaohusika na zoezi hilo kuzingatia taratibu katika kutekeleza sheria kwa wananchi walioko katika vitongoji na vijiji vilivyosajiliwa.

  Vilevile Mhandisi Makani amewataka wananchi walioko katika maeneo hayo kutoanzisha shughuli mpya za kibinadamu na kutoendelea na shughuli za kibinadamu zinazosababisha uharibifu wa mazingira na kuathiri tabia nchi.

  Wakati huohuo Mhandisi Kamani amewataka wafugaji kuondoa haraka mifugo iliyoko ndani ya maeneo yaliyoifadhiwa kisheria kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

  Mbali na hayo Serikali imewataka wananchi kutii sheria na kuepuka vitendo viovu vinavyosababisha kupotea kwa uoto wa asili kwa kasi inayoendelea nchini na kutishia uhifadhi endelevu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Serikali imeunda kikosi kazi kutafuta ufumbuzi wa kudumu katika kutatua changamoto sekta ya ardhi Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top