728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, October 22, 2016

  Rais Magufuli amteua Prof. Ninatubu Mbora Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi TAA     Prof. Ninatubu Mbora Lema

  Ikulu, Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Prof. Ninatubu Mbora Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

  Taarifa iliyotolewa leo tarehe 22 Oktoba, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 20 Oktoba, 2016.

  Prof. Ninatubu Mbora Lema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Lambert Ndiwaita aliyefariki dunia tarehe 20 Agosti, 2015.

  Prof. Ninatubu Mbora Lema ni Profesa Mshiriki Usimamizi wa Ujenzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Associate Professor of Construction Management - University of Dar es Salaam).


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  22 Oktoba, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli amteua Prof. Ninatubu Mbora Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi TAA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top