728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, October 30, 2016

  RAIS DK. MAGUFULI AMTEUA JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA TANAPA

  Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Oktoba, 2016 amemteua Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

  Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba, 2016.

  Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu.

  WAKATI HUO HUO,Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Eligy Mussa Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)
  Uteuzi wa Dkt.Shirima umeanza tarehe 29 Oktoba 2016.

  Kabla ya uteuzi huu Dkt. Eligy Mussa Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng’ombe Makao Makuu ya TALIRI.

  Jaffar Haniu
  Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  30 Oktoba, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: RAIS DK. MAGUFULI AMTEUA JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA TANAPA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top