728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, October 25, 2016

  NEWZ ALERT: MTANGAZAJI PAUL JAMES 'PJ' KUBURUZWA MAHAKAMANI NA EFM REDIO

  Mtangazaji maarufu aliyewahi kutangaza kituo cha redio cha Clouds Fm nakujiunga na EFM redio na baadaye kurudi tena Clouds Fm amefunguliwa mashtaka katika mahakama ya kazi jijini Dar es salaam na EFM redio kwa kile kinachodaiwa kuwa amekiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.

  Kufuatia mashtaka hayo, Efm inadai fidia ya shilingi milioni 200 kwa mtangazaji huyo ambaye alijiunga na kituo hicho kutoka clouds fm na baadae kudaiwa kukatisha mkataba kiholela na kurudi tena clouds fm bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake awali wakati  alipojiunga na efm redio.

  Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tarehe 23/11/2016 katika mahakama ya kazi Jijini Dar es salaam.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NEWZ ALERT: MTANGAZAJI PAUL JAMES 'PJ' KUBURUZWA MAHAKAMANI NA EFM REDIO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top