728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, October 18, 2016

  NEWZ ALERT: MAHAKAMA KUU KITENGO CHA ARDHI YATUPILIA MBALI KESI YA MBOWE HOTELS DHIDI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)

  UPDATES.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Mahakama kuu kitengo cha Ardhi imetupilia mbali kesi ya maombi ya kurejea katika jengo iliyokuwa ofisi ya Tanzania Daima pamoja na ukumbi wa Bilcanas.

  Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu katika jengo hilo.

  Amesema katika hukumu hiyo hakuna mtu aliyevunjiwa haki yake ya msingi kutokana na kufuatwa kwa Sheria dhidi ya madai ya Shirika la Nyumba NHC, kwa Mbowe HotelS.

  Wakili wa upande wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo Mbowe hotelS wanadaiwa sh. Bilioni 1.7 na NHC.Amesema vitu haviwezi kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.

  Nae Wakili upande Mbowe Hotel, John Malya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi.Amesema kuwa nakala wakiipata wanaweza kuamua katika kukata rufaa.

  Wakili wa NHC, Aliko Mwamnenge akizungumza na waandishi habari baada ya kutoka katika hukumu ya kesi iliyokuwa ikihusu maombi ya Mbowe hotels kurejea katika ofisi zake,ambapo hukumu yake imetolewa leo katika  mahakama kuu kitengo cha Ardhi,jijini Dar.
   Wakili wa Mbowe Hotels, John Malya akizungumza na waandishi wa habari juu ya hukumu iliyotelewa na Mahakama kuhusiana na maombi ya kurejea Mbowe hotels na Mali zake,  katika mahakama kuu kitengo cha ardhi leo jijini Dar es salaam.
   Mawakili wakitoka mahakamani leo mara baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa. picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi imefuta kesi iliyofunguliwa na Mbowe Hotels Ltd. dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ,kuwa Shirika hilo liliitoa kampuni hiyo katika jengo lake jijini Dar es salaam kwa kufuata taratibu zote na kuzishikilia mali zake kihalali.

  Uamuzi huo umetolewa asubuhi hii na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.

  Mlalamikaji alikuwa wakidai kwamba wakati NHC inamtoa  kwenye nyumba alikuwa ndani ya Mkataba wa Ubia na NHC, lakini Jaji alikataa hilo na kusema ingawa Mkataba wa Ubia Ulikuwepo lakini kwa kuwa haukutekelezwa ipasavyo. 

  Na wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba Walikuwa na Mahusiano ya Mwenye Nyumba na Mpangaji, Mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya Utekelezaji wake.

  Mawakili wa Mbowe Hotels Mhe. John Mallya na Mhe. Peter Kibatala (pichani ) wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa kesi ya mteja wao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NEWZ ALERT: MAHAKAMA KUU KITENGO CHA ARDHI YATUPILIA MBALI KESI YA MBOWE HOTELS DHIDI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top