728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, October 5, 2016

  NECTA WAANZISHA MFUMO MPYA WA NAMBA KWA SHULE ZA MSINGI KUONDOA TATIZO LA WANAFUNZI HEWA

    Na Humphrey Shao, Dar es Salaam

  Baraza la mitahani nchini limeanzisha mfumo mpya wa Kutunza Kumbukumbu za Wanafunzi wa shule za Msingi (PREM), Utakaosadia uandikishwaji wa wanafunzi wote.

  Akizungumza na waandishi wa habari mapema jijini Dar es Salaam leo Afisa Habari wa Baraza la Mitihani nchini John Nchimbia, alisema kuwa mfumo huo utatoa namba Maalum ambayo itamtambulisha mwanafunzi katika ngazi zote za mitihani.

  “Mfumo huu utakuwa na faida nyingi sana pamoja na kusaidia katika uhamisho wa mwanafunzi kutoka shule moja kwenda nyingine ndani ya mkoa au nje ya mkoa hivyo kuondoa tatizo la wanafunzi hewa”alisema Nchimbi.

  Aliongeza kuwa mfumo huu utasaidia katika uandaaji na utoaji wa Takwimu za Wanafunzi katika ngazi ya shule Wilaya ,Mkoa mpaka Taifa.

  Alimaliza kw akusema kuwa Baraza limeanza kufanya majaribio ya Mfumo huu katika mikoa miwili ya Mwanza na Ruvuma na Ifikapo Disemba mfumo utaimarishwa ili Januari hadi Mei 2017 utumiwe nchi nzima kwa shule za msingi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NECTA WAANZISHA MFUMO MPYA WA NAMBA KWA SHULE ZA MSINGI KUONDOA TATIZO LA WANAFUNZI HEWA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top