728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, October 13, 2016

  Mkuu wa wilaya ya Iringa azindua tiba ya kinga ya Kichocho

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela leo amezindua kampeni ya kuwanywesha watoto dawa ya Kinga tiba kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya kichocho kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani Iringa. Shule zote za msingi katika wilaya ya Iringa zitapata dawa na kuwanywesha watoto wote ilikujikinga na ugonjwa wa kichocho. 

  Mh Kasesela alisema ” wazazi wawa ruhusu watoto wao kupata kinga tiba kwani wataondokana na ugonjwa hatarishi. wataalamu wametuambia hazina madhara yoyote ili mradi mtoto awe amekula”. Shule zote zitakazo toa dawa zitahakikisha watoto wana pata chakula kabla hawajapewa.
  Zoezi hili litafanyika kwa wiki  mbili na kuhakikisha kila mtoto anapata Kinga tiba.

   Pichani mbalimbali zikionyesha Mkuu wa wilaya akiendesha zoezi la kugawa dawa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Umsalaam iliyopo manispaa ya Iringa. Pia alipatafursa ya kuwafafnunulia baadhi ya wazazi waliokuwa na shaka na dawa hizo . 
  a2 a3 a4
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Mkuu wa wilaya ya Iringa azindua tiba ya kinga ya Kichocho Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top