728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, October 24, 2016

  MKUTANO WA MAHUBIRI YA INJILI YA NABII MALISA JIJININI ARUSHA

  Kiongozi mkuu wa kanisa la Ukombozi ,Nabii B.G Malisa akihubiri katika mkutano mkubwa wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini Arusha ambapo amewatakaWatanzaniakudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kufanya matukio ambayo yanaweza kuchochea vurugu na hatari ya kuliingiza taifa katika hali ya machafuko. (Picha na Pamela Mollel).
  Kulia ni mama mchungaji Grace Mshindi wa kanisa la ukombozi tawi la Arusha akiwa anazungumza na watu waliojitokeza katika mkutano huo wa maombezi na kupokea uponyaji.
  .Watu mbalimbali waliojitokeza katika mkutano wa Kiongozi mkuu wa kanisa la Ukombozi ,Nabii B.G Malisa unaofanyika katika viwanja vya reli jijini Arusha. 
  Taswira ya watu waliojitokeza katika mkutano huo .

  Pamela Mollel,Arusha


  Watanzania wametakiwa kudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kufanya matukio ambayo yanaweza kuchochea vurugu na hatari ya kuliingiza taifa katika hali ya machafuko. 

  Wito huo umetolewa jana na mchungaji kiongozi wa kanisa la Ukombozi hapa nchini, Nabii B. G Malisa wakati alipokuwa akihubiri neno la Mungu katika viwanja vya reli jijini Arusha na kuhudhuriwa na maelfu ya watu

  Nabii Malisa alisema kwamba watanzania wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanaombea amani ya nchi iendelee kutawala kwa kuwa bila amani hakuna kitu kitakachoweza kuendelea katika nchi hii.

  Aidha alisema kuwa amekuwa akifanya ziara mbalimbali katika nchi mbalimbali duniani na kushuhudia hali ya usalama ikiwa tete ambapo askari wamekuwa wakitembea mitaani huku wameshika silaha za moto. 

  "Hivi karibuni nilikuwa Nigeria wakati nashuka uwanja wa ndege nilipokelewa na askari wenye silaha za moto nikajiuliza maswali mengi sana kuhusu amani tuliyonayo hapa Tanzania "alisema Malisa 

  Hatahivyo, alitoa wito kwa serikali kuunga mkono juhudi za viongozi mbalimbali wa dini hapa nchini katika kuwasaidia vijana na kusema viongozi wa dini wanafanya kazi kubwa katika kuwainua watu kiuchumi na kuwaepusha na vitendo viovu. 

  Awali akizungumza na waandishi wa habari mchungaji wa kanisa la Ukombozi tawi la Arusha Mchungaji Ushindi alisema kwamba mhubiri huyo atakwenda kufanya huduma ya maombezi mkoani Arusha kwa siku nane na kuwataka wakazi hao kujitokeza kwa wingi. 

  Mchungaji Ushindi alisema kuwa wakazi wa jiji la Arusha wamepata neema kubwa ya kupata neno la Mungu kupitia mkutano huo wa maombezi .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MKUTANO WA MAHUBIRI YA INJILI YA NABII MALISA JIJININI ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top