728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, October 13, 2016

  MHE: POSSI AWA MGENI RASMI MKUTANO WA WADAU WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA UWASILISHAJI WA TAFITI MPYA ZA HALI HALISI YA ULEMAVU NA UZEE NCHINI TANZANIA.

   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiwasilisha mada ya masuala ya Watu wenye Ulemavu wakati wa mkutano wa wadau wa masuala hayo walipowasilisha Matokeo ya Tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano hoteli ya Serena Dar es Salaam Oktoba 12, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  pos2
  Mkalimani wa lugha ya alama Bw.Thomas Shayo akifasiri ujumbe kwa kundi la watu wenye ulemavu (wasiosikia) uliotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum uliofanyika katika Ukiumbi wa hoteli ya Serena Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  pos3
  Mtafiti Rika Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Bi. Regina Mbaji akiwasilisha mada wakati mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum walipowasilisha matokeo ya tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini Ukumbi wa Mikutano hoteli ya Serena Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  pos4
  Mshiriki Rika (kundi la wazee) Bi.Elizabeth Nkwera akitoa mada ya usawa wa  huduma za kijamii kwa makundi maalum wakati wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum walipowasilisha matokeo ya tafiti Mpya ya Ubainishaji Hali Halisi ya Ulemavu na Uzee Nchini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  pos5
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya wadau walioshiriki katika Mkutano wa kujadili masuala ya watu wenye mahitaji maalum uliofanyika katika hoteli ya Serena Oktoba 12, 2016, wa kwanza kulia ni Bi. Clotilda Isdori na katikati ni Bw.Elisha Sibale. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  pos6
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa masuala la watu wenye mahitaji maalum ulioandaliwa na Mashirika ya misaada. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MHE: POSSI AWA MGENI RASMI MKUTANO WA WADAU WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA UWASILISHAJI WA TAFITI MPYA ZA HALI HALISI YA ULEMAVU NA UZEE NCHINI TANZANIA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top