728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, October 25, 2016

  MELI YA MV MAPINDUZI II YAREJEA ZANZIBAR  Na Kijakazi Abdalla Habari Maelezo


  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetumia kiasi ya dola 90 elfu kuifanyia matengenezo ya kawaida Meli ya MV Mapinduzi ll iliyopelekwa Chelezoni Mombasa.

  Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abuod Jumbe mara baada ya kuwasili Bandarini Malindi amesema itaanza safari zake za kawaida Pemba kuanzia kesho ili kupunguza usumbufu wa usafiri uliojitokeza baada ya kuondoaka meli hiyo.

  Alisema kuwa meli hiyo imefanyiwa matengenezo ya kawaida na hakuna kitu kilicho badilishwa na baada ya matengenezo hayo itakuwa chini ya Mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka kwa udhamini wa mtengenezaji.

  Hata hivyo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji amesema hivi sasa Serikali imo katika mchakato wa kununua meli nyengine mbili mpya, moja kwa ajili ya abiria na mizigo na nyengine itakuwa ya mafuta

  Mapema Nahodha wa Meli hiyo Abdulrahman Mzee amesema matengenezo ya meli yaliyofanyika yamekwenda sambamba na muda uliopangwa na yamefanywa kwa hali ya ubora kabisa

  Amesema kuwa kufanyika kwa matengenezo ya meli hiyo ni jambo la kawaida kwa chombo chochote cha usafiri jambo linalokipa ubora chombo husika.

  Meli ya MV Mapinduzi ll iliondoka Zanzibar wiki mbili zilizopita kwenda chelezoni Mombasa na imerejea Zanzibar leo kupitia Pemba ikiwa imechukua abiria 1200 pamoja na mizigo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MELI YA MV MAPINDUZI II YAREJEA ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top