728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, October 14, 2016

  Mbunge wa Mkuranga aendelea na ziara ya kijiji kwa kijiji kusikiliza na kutatua kero zao.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  Mkuranga.

  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, amesema kuwa anataka wananchi wamtume cha kuzungumza bunge lijalo juu ya changamoto zao.

  Hayo ameyasema katika ziara ya kijiji kwa kijiji katika vijiji Picha ndege pamoja na vikindu, amesema wananchi bila kumtuma hana cha kuzungumza.

  Amesema muda wake pasipo kuwa na Bunge utatumika katika kusikiliza kero za wananchi ambao ndio dhamana yake ya ubunge.Ulega amesema wananchi katika kutekeleza  miradi ni lazima wachangie ndipo serikali iweze kuunga mkono.

  Aidha katika changamoto ya umeme ameliomba shirika la Umeme nchini kumaliza changamoto hiyo kutokana na kusubiri kwa muda Mrefu.
   .mbunge wa mkuranga, Abdallah Ulega akitoa Maelezo kwa kaimu meneja wa tanesco juu ya kushughulikia changamoto ya umeme.
  Mbunge wa mkuranga ,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha vikindu, mkuranga.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Mbunge wa Mkuranga aendelea na ziara ya kijiji kwa kijiji kusikiliza na kutatua kero zao. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top