728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, October 9, 2016

  MBUNGE WA CHALINZE AKABIDHI MAGODORO 200 KWA SHULE YA MORETA

  Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akikabidhi magodoro kwa wanafunzi na mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Moreto ,Justine Lyamamu ,ambapo bweni la wasichana katika shule hiyo liliungua wiki iliyopita.
  Mbunge wa Chalinze Ridhiwani akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya chalinze, Mkurugenzi na maafisa wengine wa halmashauri ya Wilaya Chalinze.

  Mbunge wa chalinze ametimiza ahadi yake ya kuchangia magodoro 200 na Halmashauri ya wilaya ya chalinze kwa shule ya Sekondari ya Moreto.

  Mbunge akisema neno la ushauri na kuwatia moyo vijana kwa tukio lililowakuta na kwa utulivu uliotokea.


  Wanafunzi wa shule ya sekondari Moreto iliyopo Lugoba wilayani Bagamoyo, Mwanahamis Msonde na Sekion Mponela wakimshukuru Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu kwa msaada wa magodoro.

  Na Mwamvua Mwinyi.

  MBUNGE wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete kwa kushirikiana na halmashauri ya Chalinze,wametoa magodoro 200 yaliyogharimu zaidi ya mil.8 ili kuwasaidia wanafunzi wa shule ya sekondari ya Moreto iliyopo Lugoba wilayani Bagamoyo.

  Aidha Ridhiwani ameahidi kushirikiana na wadau pamoja na halmashauri hiyo,kujenga bweni jipya la wanafunzi wa kike,shuleni hapo baada ya kuunguliwa na bweni wiki iliyopita.
  Sambamba na hayo tathmini imebaini hasara ya sh.mil 74 baada ya bweni hilo kuungua na kusababisha mali zote kuteketea kwa moto.

  Akikabidhi magodoro hayo ,kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo,Justine Lyamuya ,mbunge huyo alisema kati ya magodoro hayo 136 yatatumiwa na wanafunzi wa kike na yatakayobaki yatatumika na wanafunzi wa kiume.

  Ridhiwani alisema mara baada ya kutokea kwa janga hilo, alitoa magodoro 50 yenye thamani ya mil.2.2 kwa nguvu zake mwenyewe.

  Hata hivyo aliwataka wanafunzi hao kushirikiana na serikali na vyombo vya dola kuwafichua waliohusika na tukio la kuchoma moto bweni.

  Ridhiwani alielezea kuwa serikali itahakikisha waliohusika kuchoma moto bweni hilo,wanatafutwa ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

  Alisema tukio hilo linasikitisha na kurudisha nyuma juhudi za serikali na wadau mbalimbali wa elimu wanaohakikisha wanafunzi wanakaa bweni .

  “Tumeweka mikakati ya kuhakikisha tunawakamata wale wote waliohusika na tukio hili baya na matukio haya ni mwendelezo wa uunguzaji wa shule ambapo Chalinze imechomwa mara mbili,” alisema Ridhiwani.

  Ridhiwani aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kushirikiana kutatua changamoto zilizojitokeza shuleni humo.

  Nae mwalimu mkuu wa shule hiyo Justine Lyamuya alifafanua kuwa vitu vyote viliungua ikiwa ni pamoja na vitanda na magodoro 75 vyenye thamani ya mil. 24.

  Alisema bweni hilo lilijengwa hivi karibuni kwa thamani ya mil.50 ambalo limeungua lote na halifai tena kutumika.

  “Moto huo uliunguza vitu vyote vilivyokuwemo ikiwepo magodoro, vitanda 75, madaftari, vitabu, nguo na vifaa vingine lakini mungu alisaidia kati ya wanafunzi 196 wanaolala bweni hili,hawakuwepo bwenini,” alisema Lyamuya.

  Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze,Said Zikatimu alisema licha ya kuchangia magodoro hayo tayari wameitisha kikao na wazazi, walezi na wadau wa elimu ili kujadili namna ya kukabiliana na tatizo hilo.

  Baadhi ya wanafunzi Sekion Mponela na Mwanahamis Msonde walimshukuru mbunge wa Chalinze na halmashauri kwa msaada walioutoa na kuahidi kutunza magodoro hayo.

  Octoba 5 mwaka huu majira ya asubuhi moto ulizuka katika bweni la wanafunzi wa kike shuleni humo na kusababisha hasara kubwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MBUNGE WA CHALINZE AKABIDHI MAGODORO 200 KWA SHULE YA MORETA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top