728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, October 8, 2016

  MBUNGE ULEGA AZINDUA KISIMA CHA KISASA KATIKA KIJIJI CHA LUPONDO ,MKURANGA

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii,Mkuranga 

  MBUNGE wa Mkuranga, Abdallah Ulega, amezindua kisima katika Shule ya Msingi Lupondo, kilichojengwa na African Reflection Foundation. 

  Akizungumza Mara baada ya kuzindua Kisima hicho, amesema kuwa kijiji cha Lupondo kilikuwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu. Amesema kuwa wananchi hao walikuwa wakitafuta maji umbali wa kilomita tano na kufanya kuumiza kichwa katika kuwapata wafadhili wa mradi huo. 

  Ulega amesema katika kipindi cha miezi tisa ameweza kupata miradi ya maji katika vijiji sita na kuahidi kuendelea kutafuta miradi ya maji katika vijiji vilivyosalia.Hata hivyo katika uzinduzi huo Mh.Ulega ametoa msaada wa mifuko 10 ya saruji katika msikiti wa kijiji hicho. 

  Nae mratibu wa African Reflection foundation, Shiraz Mohamed, amesema wataendelea kufadhili miradi ya maji katika vijiji vyenye changamoto hiyo. 
  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega,(katikati) akikata utepe wa uzinduzi wa kisima jana katika kijiji cha Lupondo.
  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Lupondo jana mkoa wa Pwani
  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lupondo kabla ya uzinduzi wa kisima cha maji katika kijiji cha Lupondo jana mkoa wa Pwani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MBUNGE ULEGA AZINDUA KISIMA CHA KISASA KATIKA KIJIJI CHA LUPONDO ,MKURANGA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top