728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, October 1, 2016

  MAZOEZI YA SERENGETI BOYS WAKIJIANDAA NA MCHEZO WA JUMAPILI DHIDI YA CONGO BRAZAVILLE

  Libero wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Ally Msengi (Kulia) akimiliki mpira huku Mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Abdallah akipigia hesabu mpira huo wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili. 
  bra6
  Baadhi ya vigogo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, kutoka kushoto ni Dk. Gilbert Gilbert Kigadye, Mratibu wa timu, Pelegrinus Rutayuga na Dk. Sheicky Mngazija wakifuatilia mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
  bra7
  Kipa Na. 1 wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
  bra1
  “CONGO TUTAWAZIKA HAPA”Ndivyo anavyoonekana kusema Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo. Uwanja huo ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville ndio utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Congo, Jumapili Oktoba 2, 2016.
  bra2
  Huyo ndiye Muhsin Malima Makame au unaweza ukamwita ‘Super Sub’ wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, akikokota mpira kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kuonyesha uwezo wake uwanjani pindi anapoingia kipindi cha pili kuokoa jahazi. Akikosa kufunga huwa ni kama bahati mbaya.
  bra3
  Beki wa kushoto wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Nickson Kibabage akimdhibiti Kelvin Nashon wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
  bra4
  Kiungo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Kelvin Nashon ‘akisepa na kijiji cha mabeki’ wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAZOEZI YA SERENGETI BOYS WAKIJIANDAA NA MCHEZO WA JUMAPILI DHIDI YA CONGO BRAZAVILLE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top