728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, October 28, 2016

  MATOKEO YA DARASA LA SABA 2016 SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAJIPONGEZA KUFANYA VIZURI


  Mwanafunzi aliyeongoza masomo yote Rahma Mdeka akipokea cheti cha kuhitimu darasa la saba na zawadi yake wakati wa mahafali ya shule ya Southern Highlands Mafinga
  Mkurugenzi wa shule za Southern Highlands Mafinga ,Mary Mungai kulia akitambulisha watumishi wa shule hiyo.
  .........................................................................................................

  Na MatukiodaimaBlog

  UONGOZI wa shule ya Southern Highlands Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani umeeleza kufurahishwa na matokeo ya mtihani wa darasa la saba Taifa baada ya wanafunzi wote 51 waliofanya mtihani huo kufaulu na kuifanya shule hiyo kushika nafasi ya kwanza Kiwilaya .

  Pamoja na kuongoza kiwilaya pia shule hiyo ya Southern Highlands Mafinga imekuwa shule ya 6 kati ya shule 232 katika mkoa wa Iringa na shule ya 198 kati ya shule 8109 kitaifa .Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Mary Mungai akizungumza leo kufuatia matokeo hayo alisema kuwa pamoja na kuwa shule hiyo haijapata kufelisha mwanafunzi hata mmoja toka ilipoanzishwa 2001 ila bado ana imani jitihada zaidi zitaongezwa ili kuzidi kushika nafasi za juu zaidi kimkoa na kitaifa .

  “ Ni jambo la kumshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye Kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo kila mwaka wanafunzi wote wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari....ni matumaini yetu imani kwa wazazi inazidi kuongezeka zaidi kwa shule yetu"Alisema kuwa toka shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya vizuri na hakuna mtoto aliyepata kufeli .

  “Shule yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza”

  Alisema katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza. Aidha alisema kwa mwaka huu 2016 jumla ya wanafunzi 51 walisajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba na wote walifanya wastani wa shule 185.3137 kundi la shule watahiniwa 40 au zaidi ambapo imeweza kuongoza kiwilaya kuwa ya kwanza na kimkoa ya 6.

  Mkurugenzi huyo alisema kuwa ajili ya kuwashukuru wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule hiyo wameamua kutoa punguzo ya ada kwa wanafunzi hao waliofaulu mtihani wa darasa la saba ambao watajiunga na shule ya Sekondari ya Southern Highlands Mafinga ,huku akiwaomba wazazi wenye watoto wanaohitaji kujiunga na shule hiyo kuwapeleka watoto wao kwani shabaha kuu ni kuona watoto wanaendelea kupata elimu bora.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MATOKEO YA DARASA LA SABA 2016 SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAJIPONGEZA KUFANYA VIZURI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top