728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, October 22, 2016

  KINGATIBA ZA MATENDE, MABUSHA NA MINYOO KUANZA KUTOLEWA OKTOBA 25

  Na Ally Daud- MAELEZO

  SERIKALI kupitia mpango wa Taifa Wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele itaanza kugawa kingatiba za ugonjwa Wa matende, mabusha na Minyoo Oktoba 25 mwaka huu ili kuondoa kabisa magonjwa hayo mpaka ifikapo 2020.

  Akizungumza hayo katika semina na waandishi Wa habari kuhusu magonjwa hayo Afisa Mpango wa huduma hiyo Bw. Oscar Kaitaba  amesema kuwa zoezi hilo litaanza Oktoba 25 hadi Oktoba 30 mwaka huu katika maeneo yote ya Dar es salaam.

  "Zoezi la kugawa kingatiba kwa wananchi Wa Dar es salaam litaanza Oktoba 25 na kumalizika Oktoba 30 ili kuweza kupambana na vimelea vya magonjwa hayo na kuendelea na mikoa mingine" alisema Kaitaba.
  Aidha Bw.Kaitaba amesema kuwa kingatiba ambazo zitatolewa ni Ivermectin na Albendazole ili kuondoa magonjwa ya Matende,Mabusha, na Minyoo kwa wakazi wa Dar es salaam na vitongoji vyake.

  Bw.Kaitaba amesema kuwa kingatiba hizo zitatolewa kwa wananchi wote wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea katika maeneo yote ya Dar es salaam katika stendi za mabasi, Masoko,Hospitalini, Ofisi za Serikali za Mitaa, Ofisi za Wizara, Kambi za majeshi ns Magereza.

  Aidha Bw.Kaitaba ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa wajitokeze kwa wingi kupata kingatiba hizo wakiwa wameshakula vizuri chakula na kuondokewa na imani potofu kwamba zinachangia kuzuia mimba ama kwa wanaume kupungukiwa nguvu za kiume.

  Kwa upande wake Muhamasishaji Wa Mpango huo kutoka Wizara ya Afya Bw. Makora Said amesema kuwa Semina hiyo inahusu kuwahamasisha waandishi wa habari kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Mpango Wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini kama vile Matende, Mabusha, Minyoo, Usubi, Trakoma na Kichocho.

  Aidha Bw. Makora amesema kuwa kama waandishi watakavyoielimisha jamii kwa elimu ya kutosha na wananchi wakakubali wito Wa kutumia kinga tiba hizo Serikali itafanikiwa kuepusha ulemavu na udumavu kwa watanzania.

  Aidha Bw. Makora amesema kuwa waandishi wanatakiwa wawe kipaumbele katika kuandika habari za afya ya Binadamu ili kuwapa ufahamu  wananchi na uwezo Wa wa kufanya maamuzi sahihi juu ya afya zao kwa ujumla.                  
        
  Semina hiyo ya siku moja imelenga kuwaelimisha waandishi Wa habari kuhusiana na Mpango Wa Kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ili elimu ya kutosha ikatolewe kwa wananchi ili kufanikisha lengo la Sera ya Afya ya mwaka 2007 hadi kufikia 2020.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KINGATIBA ZA MATENDE, MABUSHA NA MINYOO KUANZA KUTOLEWA OKTOBA 25 Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top