728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, October 14, 2016

  Kampuni ya SBC Tanzania (PEPSI) yatoa wito makampuni kusaidia zaidi watoto wenye mahitaji maalum


  Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Spur, Bw. Lokesh Marakala (Wapili Kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Zinga Amani, Bi. Margareth Mwegalawa (kulia), vitu mbali mbali viliyotolewa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI) kusaidia kituo hicho kilichopo Bagamoyo katika hafla fupi hivi karibuni. Kulia ni Meneja Masoko wa SBC Tanzania Limited (PEPSI) Bi. Roselyne Kwelukilwa
  Wafanyakazi wa SBC Tanzania Limited (PEPSI) na Spur katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha watoto yatima cha Zinga Amani, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vitu mbali mbali vilivyotolewa na kampuni hizo mbili kusaidia kituo hicho kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani
  Meneja Msoko wa kampuni ya SBC Tanzania (PEPSI) Bi. Roselyne Kwelukilwa (Kushoto) akiwapatia watoto wa kituo cha watoto yatima cha Zinga Amani chakula wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vitu mbali mbali vilivyotolewa na kampuni hizo mbili kusaidia kituo hicho kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.
  Watoto hao wa kituo cha watoto yatima cha Zinga Amani kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani wakiwa katika mchezo wa kuvuta kamba.


  Dar es Salaam.

  Kampuni ya vinywaji baridi ya SBC Tanzania Limited (Pepsi) imetoa msaada kwa watoto yatima 38 wanaolelewa kwenye kituo cha kulea watoto yatima cha Amani kilichopo Zinga, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

  Kwa kuwa Serikali peke yake haiwezi kukabiliana na changamoto watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu, hatuni budi kufanya jitihada za makusudi kupunguza changamoto hizo, amesema Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Roselyne Kwelukilwa.

  “Ndio sababu, kampuni ya Pepsi imekuwa mstari wa mbele wa kusaidia jamii kwa kuhakikisha watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu wanapata elimu na huduma nyingine za msingi”, asema meneja huyo.

  " Watoto wanahitaji upendo, haki ya kupata elimu bora na kushiriki kwenye michezo ili kuwa na afya njema na kuboresha uelewa darasani,” ameendelea kusema Kwelukilwa.

  Pepsi kwa kushirikiana na wateja wao, Spurs, ambao wanaendesha migahawa ya chakula katika zaidi ya nchi 15 duniani, ilitoa vifaa na msaada mbali mbali ikiwemo kilo 300 za mchele, nguo, vifaa vya elimu, vitabu, viatu, meza ya kuchezea mpira (soccer table) na vikaragosi (toys) .

  “Kampuni ya Pepsi, kupitia kitengo cha kusaidia jamii tumekuwa tukisaidia jamii tunayofanya nayo kazi, kwani ndio wadau wetu wa biashara ya vinjwaji baridi na inatupasa kurudisha kwa jamii sehemu ya faida yetu kwa kuwa ndio inayotuwezesha,” amesema Kwelukilwa.

  SBC Tanzania Limited (Pepsi) hivi karibuni wamemkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa mchango wa milioni 50 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kager mwezi ulipita. Pia wamechangia Shilingi milioni 20 kwa ajili ya kutengeneza madawati ya shule mkoani Shinyanga na wametoa madawati 200 mkoani Dar es Salaam.

  Naye Lokesh Marakala, meneja uendeshaji wa Spurs amesema kuwa watoto yatima na walio katika mazingira magumu wanahitaji msaada ili wajisikie kuwa ni sehemu ya jamii.“ Tunashirikiana na wadau wetu, wakiwemo kampuni ya Pepsi kusaidia jamii, ndio maana kila mwezi, tunatoa msaada kwa vituo vitatu vya watoto watima,” amesema meneja huyo.

  “Chakula ni sehemu ya msaada tunaotoa kwa sababu, kile chakula kizuri tunachouza, kinastahili pia kuliwa na watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu,”amesema Marakala kutoka kampuni hiyo ya Afrika ya Kusini.
   
  “ Hii ni mara ya pili kutoa msaada katika kituo hiki cha Amani kwa kushirikiana na Pepsi, mara ya mwisho tulisaidia kujenga jiko la kisasa, yaani nyumba kwa ajili ya kupika chakula, badala ya nyumba ya tope waliyokuwa wakiitumia hapo awali,”Amehitimisha Marakala.

  Mkurugenzi wa kituo hicho, Margareth Mwegalawa aliishukuru kampuni ya SBC Tanzania Limited (Pepsi) na Spurs kwa msaada wao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  1. Do you prefer Pepsi or Coke?
   PARTICIPATE IN THE POLL and you could get a prepaid VISA gift card!

   ReplyDelete

  Item Reviewed: Kampuni ya SBC Tanzania (PEPSI) yatoa wito makampuni kusaidia zaidi watoto wenye mahitaji maalum Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top