728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, October 31, 2016

  IDARA YA ANGA YA ETIHAD KUTOA FURSA ZA AJIRA 425,000 AFRIKA.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Idara ya anga ya Etihad, James Hogan

  IDARA ya anga ya Shirika la ndege la Etihad kwa kushirikiana na wadau wake, wanatarajia kutoa takriban fursa 425,000 za ajira ikiwa ni pamoja na kutoa Dola za Marekani 3.6 milioni kwa lengo la kuinua uchumi wa Afrika mwaka 2016, fursa hiyo inatolewa kufuatia kukua kwa mji wa Abu Dhabi katika sekta ya biashara ya usafirishaji nje na ndani ya mji huo.

  Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Uchumi ya Oxford, inabainisha kwamba Idara hiyo ya anga pamoja na wadau wake wana mchango mkubwa katika kukuza uchumi barani Afrika na duniani kote ikiwa ni pamoja na kuunganisha vituo vya biashara na masoko yaliyopo.

  Taarifa hiyo inaeleza kwamba,Idara hiyo ya anga (EAG) na wadau wake wanatarajia kuchangia dola za Marekani1.1 bilioni katika uchumi na Sekta ya Utalii dola 2.5 bilioni. Licha ya hiyo, zitatolewa ajira 117,000 na zingine 308,000 katika sekta ya utalii.

  Kwa Mwaka huu wa 2016, Shirika la ndege la Etihad linahudumia jumla ya vituo 117 vya abiria na pamoja na mizigo duniani kote. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kufikia abiria 19 milioni watakao hudumiwa kwa zaidi ya ndege 100,000 ambazo kati ya hizo, ndege 8,300 zitafanya safari za Amerika kwa abiria 1.1 milioni kutoka duniani kote.

  Tangu kuzinduliwa kwa safari yake ya kwanza kwenda Misri mwaka 2004, Etihad imepanua wigo wa huduma zake barani Afrika, sambamba na ufunguzi wa vituo vingine zaidi katika nchi nane zingine zikiwamo Afrika Kusini, Morocco, Libya, Sudan, Kenya, Nigeria, Uganda na Tanzania.

  Kiasi cha dola 1.1bilioni kilichotolewa, kinatokana na shughuli zinazofanywa na idara hiyo ya anga duniani kote,pamoja na  mchango wa wadau wake. Katika mchango huo, Idara ya anga pekee inatarajiwa kuchangia dola 400 milioni na fursa za ajira 3,900 mwaka huu. Kiasi hicho cha fedha kwa sehemu kubwa kitategemea   bidhaa zitakazo uzwa barani Afrika.

  Afisa mtendaji mkuu wa idara ya anga ya Etihad, James Hogan amesema “ fursa za ajira zilizotolewa  katika  utalii, sekta ya usafirishaji, na huduma za vyakula zinatokana na uwepo wa idara ya anga ambayo imetoa fursa mbalimbali za ajira katika soko letu la Afrika, pia ni ishara ya kukua kwa sekta ya usafirishaji kupitia kitovu chetu cha biashara cha Abu Dhabi.”


  Jumla ya wageni 1.1 milioni wanatarajiwa kuitembelea Afrika kupitia Shirika la Etihad na wadau wake mwaka huu. Wageni hao wanatarajiwa kukuza pato la Afrika kupitia sekta mbalimbali, ambapo pato la Afrika litaongezeka kufikia dola 2.5 bilioni sambamba na ajira 308,000 ifikapo mwaka 2024. 

  Idadi ya wageni watakao wasili Afrika inatarajiwa kuongezeka na kuwa zaidi ya watu 3.2 milioni, ambapo idadi hiyo itakuza uchumi kufikia dola 5.6 bilioni na ajira 596,000.

  Aidha, ripoti imeonesha namna faida iliyopatikana kutokana na kuimarika kwa huduma za anga zinazotolewa na Etihad zilivyoingizwa katika bajeti ya barani Afrika, juhudi hizi zinalenga kukuza uzalishaji ambao ni sawa na dola 1.1 bilioni kwa mwaka huu, ikiwa ni sawa na ajira 72,200. Hata hivyo, uzalishaji unatarajiwa kuongezeka kufikia dola 2.2 bilioni ifikapo 2024 ambapo ni sawa na ajira 145,000.

  Idara ya anga alianzishwa mwaka 2014, ikiwa na vitengo vinne vya Shirika la Etihad, Uhandisi, kikundi cha Hala na wanahisa. Idara pia imewekeza katika mashirika saba ya ndege ambayo ni Air Berlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia, na Darwin Airline ya Uswisi, ambayo inafanya kazi kama sehemu ya Etihad.  

  Hogan aliongeza kuwa, “wadau wetu ni sehemu muhimu ya kuendeleza shughuli zetu Afrika, tunawashukuru kwa ushirikiano wanao uonesha na tuko tayari kuitumikia Afrika kifanisi zaidi. Wadau wetu pia  ni sehemu muhimu ya kuimarisha shughuli zetu”
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: IDARA YA ANGA YA ETIHAD KUTOA FURSA ZA AJIRA 425,000 AFRIKA. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top