JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


HUAWEI YACHANGIA KATIKA SEKTA YA ELIMU YA TANZANIA.

Share This
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi  kutoka kwa Naibu Balozi wa China kwa Tanzania Bw. Gou Haodong (wa pili kulia) wakati wa hafla ya kukabidhi mchango iliyoandaliwa na Ubalozi wa China kwa kushirikiana na Huawei Tanzania kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam jana. Wanaoshuhudia (wa kwanza kulia) ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bruce Zhang.
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifanya mazungumzo na Naibu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Gou Haodong kabla ya hafla ya makabidhiano ya mchango  wa Milioni 60 kwa ajili ya maafa ya Kagera sambamba na Milioni 220 kwa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya mradi wa Huawei ‘Seeds for the future’ maalum kwa ajili ya kuwapeleka wanafunzi 10 bora wa vyuo vikuu nchini China kujifunza masuala ya TEHAMA. Msaada huo ulitolewa na Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kushirikiana na Huawei mapema jana jijini Dar es Salaam. (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bruce Zhang.
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji Huawei Tanzania Bruce Zhang mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam mapema asubuhi ya jana kwa ajili ya kuzindua programu ya Huawei ‘Seeds for the future’ ambapo alikabidhiwa kiasi cha Milioni 220 kwa ajili ya programu hiyo na milioni 60 kwa ajili ya maafa ya Mkoa wa Kagera. Pamoja naye (Toka kushoto) ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga na Naibu Balozi wa China nchini Tanzania Gou Haodong. 
Picha ya Pamoja 

Huawei, moja ya Kampuni inayoongoza ulimwenguni katika utoaji wa huduma ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA), siku ya jana imeimarisha mchango wake katika sekta ya elimu ya Tanzania.

Katika hafla ya makabidhiano iliyoandaliwa na Ubalozi wa China kwa kushirikiana na Kampuni ya Huawei leo hii, Kampuni hiyo ilitangaza kuwa programu yake ya ‘Seeds for the Future’ ambayo ni programu kubwa na muhimu zaidi katika uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii itawafaidisha wanafunzi wengine 10 nchini  kwa mwaka 2017, ambapo sambamba na hilo Kampuni hiyo imechangia Sh milioni 60 ambazo zitaisaidia Serikali katika kukarabati baadhi ya Shule zilizokumbwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera hivi karibuni na milioni 220/- iliyoelekezwa kwenye Wizara ya elimu kwa ajili ya programu ya Huawei ‘Seeds for the future’.

Akizungumza katika hafla, hiyo Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, aliipongeza Huawei kwa kukuza vipaji vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini, na kuwa mstari wa mbele katika uwajibikaji kwa jamii.

Alisema Huawei imekuwa mshirika mkubwa katika sekta ya maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Tanzania na imekuwa ikiendelea kuisaidia serikali ya Tanzania katika uvumbuzi wa sekta hiyo wakati ambapo serikali inafanya juhudi ya kurekebisha kuikuza sekta hiyo kupitia miradi mbalimbali.

 “Napenda nitoe pongezi zangu za dhati kwa kampuni ya Huawei kwa kuwezesha kukuza sekta ya mawasiliano Tanzania na kwa mchango wa katika sekta ya elimu kwa kuja na programu hii mpya inayowawezesha wanafunzi kwenda kujifunza masuala ya teknolojia nchini. Ni matumaini yangu kuwa ushirikiano baina ya serikali na kampuni ya Huawei utaendelea katika sekta hii kwa kuwa sasa ina mpango wa kuanzisha elimu ya kieletroniki kwa shule za sekondari,” alisema.

“Napenda kuwahakikishia kuwa sisi kama serikali tutashirikiana moja kwa moja na Huawei kuboresha sekta ya elimu hasa katika masuala ya TEHAMA,” alisema.
Mhe Majaliwa aliongeza kuwa serkiali iko tayari kujifunza kutoka kwa Serikali ya jamhuri ya watu wa China  na Huawei kwa kuwa mengi tunatarajia kutoka kwao na kwamba Serikali itaendelea kushrikiana na Huawei katika miradi mbali mbali ya TEHAMA.

Naye Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipokea mchango wa Huawei kwa ajili ya ukarabati wa shule zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi hivi karibuni mkoani Kagera alisisitiza umuhimu wa kukuza vipaji katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Tanzania.
Alisema kuwa sekta hii ina jukumu kubwa katika maendeleo ya Tanzania kufikia kipato cha kati. Nchi zote zilizoendelea zimewekeza vilivyo kwenye sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nah ii ndio sababu muhimu ya wao kufanya vizuri kwenye Nyanja mbalimbali za kimaendeleo. Kamwe hatuwezi kufikia nchi za kipato cha kati bila kuwekeza na kukuza vipaji vya Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

“Napenda niwashukuru Huawei kwa kuanzisha mpangoi huu wa ‘Seeds for the Future’ kwa wanafunzi wa kitanzania. Kupitia katika shuhuda za ambao walishriki program hii, naweza kusema kuwa ni program hii ni muhimu sana. Na ninapenda niwahakikishie kuwa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi itaendelea kushirkiana na Huawei, kwa kuwa tumetambua kuwa setka ya TEHAMA ni muhimu katika kusaidia elimu,” alisema.

“Tunaamini kuwa sekta ya mawasiliano ina mchango mkubwa kusaidia elimu kwa kupunguza upungufu wa walimu nchini. Kwa sasa Huawei wako katika hatua za mwisho za kuanzisha mradi wa elimu ya kielektroniki na utaanza klutumia kwa shule za sekondari hivi karibuni,’ aliongeza.

Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong, alielezea kuhusu urafiki wa muda mrefu kati ya China na Tanzania.
Alisema "China na Tanzania zimekuwa zikisaidiana katika nyakati zote za raha na tabu, na kuwa Msaada uliotolewa leo na Huawei umethaminisha urafiki huo. Tunaamini kwamba Huawei, kama Kampuni inayoongoza kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kimataifa, itatumia ujuzi wa teknolojia yake ya hali ya juu katika kukuza sekta hii ya Teknolojia na Mawasiliano”.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bruce Zhang, alitoa wito wa ushirikiano wa karibu baina ya Sekta ya umma na binafsi akisema kuwa;-"Huawei itaendelea kuleta ubunifu zaidi kwenye sekta ya Teknolojia na Mawasiliano nchini  ili kuiunganisha Tanzania iliyo bora na kuleta fumbuzi mbalimbali za elimu kupitia mitandaoni na kukuza vipaji zaidi kwa Tanzania.
Bw. Bruce pia alizungumiza mbali na kuzindua muhula mwingine wa program ya Seeds for the Future pia wameungana na Ubarozi wa China kutoa msaada wao kwa waathirka wa tetemeko la ardhi lililotokea mapema Septemba hii.

“Tumeguswa sana na janga walilopata wenzetu wakazi wa mkoa wa Kagera, na tumefanya juhudi zetu zote tuwezavyo kuwasaidia ikiwemo kuongeza mifumo ya mawasiliano ambayo itawasaidia waathirika wa tetemeko hilo ili waokoaji waweze kuwa na mawasiliano bora ili kuleta ufanisi katika zoezi la uokoaji ambapo kampuni ya Huawei imetoa kiasi cha Sh60 milioni kusaidia marekebisho ya shule zilizoharibiwa na tetemeko hilo,” alisema.

Aliongeza kuwa Programu ya ‘Seeds for the future’ ya Huawei ni mradi mkubwa zaidi kimataifa katika uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii. Kwa kupitia programu hiyo Huawei Tanzania imeweka utaratibu wa kuhakikisha wanafunzi 100 wanaosomea TEHAMA katika vyuo vya hapa nchini wanafaidika na mradi huo ambapo kila mwaka wanafunzi 10 wanapata fursa ya kutembelea Beijing, China na kufanya kazi ndani ya makao makuu Huawei yaliyopo Shenzhen nchini China. Kwa mwaka 2016, wanafunzi bora 10 wanaosoma TEHAMA walinufaika na mradi huo ambapo wawili (2) kati yao wamekwisha ajiriwa na Huawei Tanzania.

Mmoja wa wanafunzi waolishirki katika mafunzo ya Seeds for the Future’ Ahmed Sufiani kutoka Zanzibar alipongeza kuanzishwa kwa program hii na kuongeza kuwa imemsaidia yeye binafsi kujiajiri kwa kufungua kampuni inayojihusisha na masuala ya TEHAMA huko Zanzibar.

Kufikia mwishoni mwa mwaka 2015, Programu hiyo ilikuwa imeshatekelezwa katika nchi 67 duniani kote, ambapo kwa mwaka huu wa 2016, Mradi huo umejipanga kuandaa wanafunzi angalau 1,000 kutoka nchi zaidi ya 70 duniani kutembelea China kwa ajili ya mafunzo ya TEHAMA.

Ni kutokana na historia kama hizi ambapo kwa mwaka jana, Serikali na Huawei zilisaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) katika kushirikiana kwenye masuala ya TEHAMA, ambapo Huawei ikiwa Kampuni rasmi ya ushauri kwa Serikali ya Tanzania kwenye masuala ya TEHAMA. Kampuni pia ilipata tuzo bora ya uongozi kwa mchango wake wa masuala ya TEHAMA nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad