728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, October 14, 2016

  GOLF LUGALO YAWASILI ARUSHA KWA AJILI YA ARUSHA OPEN

  Na Luteni Selemani Semunyu Arusha.

  Wachezaji wa timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wamewasili salama jijini Arusha na wamefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Gymkana utakaotumika kwa ajili ya michuano ya wazi inayotari wa kuanza kesho jumamosi.

  Wachezaji hao ambao wanafikia 14 wakiwemo wanawake watatu wanawake wamesema ni matumaini yao kurejea na ushindi mnono ili kuwapa faraja mashabiki wa klabu yao ambao wanamatumani makubwa nao.

  Kwa upande wake bingwa wa Moshi Open mashindano yaliyomalizika hivi karibuni kutoka Lugalo Nicholous Chitanda amesema anajivunia kuwa na mwalimu mzuri hivyo atatumia mafunzo mazuri aliyopata kutoka kwa mwalimu wake kutetea ubingwa aliopata Arusha Open katika kundi lake.

  Kwa upande wake mkuu wa msafara wa timu ya Lugalo Kapteni Amanzi Mandengule amesema kikosi chote cha timu ya Lugalo kimefika salama hakuna majeruhi na wachezaji wana ari kubwa ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka klabu ya Gymknana ya Arusha ambao ndio wenyeji wa michuano hii ya Arusha Open mwaka 2016 jumla ya washiriki 102 wamethibitisha kushiriki.

  Wachezaji hao kutoka klabu ya jeshi ya Lugalo ni 14,wawili toka mkoani Morogoro,16 kutoka klabu ya TPC ,nane kutoka klabu ya Gymkhana ya Dar es salaam, saba toka Moshi na wenyeji kutoka klabu ya Gymkhana ya Arusha 55.

  Mashindano ya wazi ya Arusha Open yanatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kwa kuanza na jumamosi na jumapili ambapo mara baada ya kumalizika kwa michezo sherehe ya ugawaji zawadi kwa washindi itafanyika kwa makundi yote ambayo ni A,B,C Senior,Junior,na wanawake
   WACHEZAJI WA KLABU YA GOLF YA LUGALO WAKIJADILIANA JAMBO WAKATI WAKIFANYA MAZOEZI KABLA YA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN YANAYOTARAJIA KUFANYIKA OKTOBA 15 NA 16 MWAKA HUU JIJINI ARUSHA .
  MPIGA GOLF NICHOLOUS CHITANDA WA KLABU YA GOLF YA LUGALO AKIWA KATIKA MAZOEZI KUJIANDAA NA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN YANAYOTARAJIWA KUFANYIKA OKTOBA 15 NA 16 JIJINI ARUSHA (PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)
  AFISA TAWALA WA KLABU YA LUGALO KAPTENI AMANZI MANDENGULE MWENYE FULANA NYEUPE AKIJADILIANA JAMBO NA MCHEZAJI MWENZIE WA KLABU HIYO PROSPER EMANUEL (KULIA) NA JUMA LIKULI( KUSHOTO )KATIKA MAZOEZI YA KUJIWINDA NA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN .
  WACHEZAJI WA KLABU YA GOLF YA LUGALO WAKIJADILIANA MATOKEO WAKATI WAKIFANYA MAZOEZI KABLA YA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN YANAYOTARAJIA KUFANYIKA OKTOBA 15 NA 16 MWAKA HUU JIJINI ARUSHA (PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: GOLF LUGALO YAWASILI ARUSHA KWA AJILI YA ARUSHA OPEN Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top