728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, October 12, 2016

  DC Mjema atoa wiki tatu wananchi kupewa hati zao.


  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, akizungumza na wakazi wa kata ya Msongola katika ziara za kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika wilaya hiyo.
   Mtendaji mkuu wa Kampunia ya upimaji na uuzaji Viwanja ya Tanzania Remex, Ali Hamadi, akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa kata ya Msongola ramaninya mipango miji katika eneo hilo .
  Katibu tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro, akizungumza na wananchi wa Kata ya Msongola wakati wa ziara ya kutatua kero za wananchi katika maeneo yao . 

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

  MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesikiliza kero 126 za wananchi wakati wa ziara yake katika kata tatu za Vingunguti, Pugu, Gongolamboto na Msongola na kuipa wiki tatu kampuni ya Tanzania Remix kuwapatia wananchi hati zao za viwanja.

  Mjema amesema kuwa wananchi hao wamesubiri kwa miaka mitatu sasa juu ya mpango huo bila kuona matumaini, hivyo hakuna haja ya kuendelea kusubiri.

  "Sasa natoa wiki tatu kuhakikisha fidia za wenye viwanja zinapatikana na baada ya wiki mbili kila mmoja awe amepatiwa hati yake ambayo itamuwezesha kuuza au kukopa katika mabenki mbalimbali"amesema Dc Mjema.

  Dc Mjema pia alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ulinzi katika kata ya Msongola kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uporaji na mauaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DC Mjema atoa wiki tatu wananchi kupewa hati zao. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top