728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, October 10, 2016

  DC KASESELA ASIFU KAZI ZA LASWA IRINGA,ATAKA MATAPELI WA MIKOPO YA RIBA KUBWA WAFICHULIWE


  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akifungua warsha ya LASWA katika ukumbi wa chuo kikuu huria cha Tanzania .

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Kasesela Kushoto akipokelewa na mkurugenzi wa LASWA Francis Mwilafi

  Mkuu wa wilaya na viongozi mbali mbali wa LASWA na Halmashauri


  Dr Theoboro Kipilimba mwenyekiti wa bodi ya Laswa akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi
  Madiwani wa Manispaa ya Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tano kulia pamoja na viongozi wa Laswa na wale wa Halmashauri za Manispaa na Iringa
  Madiwani wa Halmashauri ya Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tano kulia pamoja na viongozi wa Laswa na wale wa Halmashauri za Manispaa na Iringa
  Madiwani wa Halmashauri ya Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tano kulia pamoja na viongozi wa Laswa na wale wa Halmashauri za Manispaa na Iringa

  maofisa Watendaji wa Halmashauri ya Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Iringa
  Wafanyakazi wa Laswa wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa


  DC Kasesela akiteta jambo na Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Bw Lyata  Na MatukiodaimaBLOG

  SERIKALI wilayani Iringa imepongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na kituo cha msaada wa kisheria cha LASWA mkoani Iringa na kutaka kituo hicho kuendelea kupeleka vijijini wasaidizi wa kisheria ili kuwasaidia wananchi kujua haki zao na kuagiza wananchi kuwafichua matapeli wanaokopesha wananchi mikopo ya riba kubwa .

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha ya ufunguzi wa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wananchi wote hasa kina mama wajawazito iliyotolewa kwa madiwani wa wilaya nzima ya Iringa na watendaji wa kata jana katika ukumbi wa chuo kikuu huria cha Tanzania , mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa kumekuwepo na utapeli unaofanywa na baadhi ya watu kupitia mikopo hiyo kwa kuwatoza wananchi riba kubwa jambo ambalo halitavumiliwa .

  Kwani alisema kuwa kumkopesha mwananchi mkopo si kosa ila pale inapotokea mkopeshaji kumtaka mwananchi huyo kulipa riba mara mbili ama tano ya mkopo aliokopa ni sawa na utapeli hivyo wananchi wasisite kuwafichua wale wote wanaofanya utapeli wa aina hiyo .

  " Nawaagiza wale wote wanaofanya utapeli wa kukopesha wananchi mikopo ya riba kubwa kuacha mara moja vinginevyo nitawashughulikia kwa kuwachukulia hatua kali ......haiwezekani wananchi kuendelea kuumizwa na mikopo hiyo na baadhi yao kupokonywa nyumba zao kwa kushindwa kulipa riba kubwa wanazodaiwa "

  Mkuu huyo wa wilaya alitaka LASWA kupitia wasaidizi wake wa kisheria mijini na vijijini kuendelea kuwasaidia wananchi ambao wananyanyasika kwa kutojua sheria pamoja na kutetea wale wote wanaokandamizwa na matapeli hao wa mikopo hiyo ya riba kubwa .

  Kuhusu watendaji wa serikalini na baadhi ya mahakini wa mahakama za mwanzo zilizopo vijijini wanaotumika kuwakandamiza wananchi wasiojua sheria mkuu huyo alitaka kila diwani kufikisha taarifa ofisini kwake ili mahakimu hao na watendaji wanaopindisha sheria kwa kujinufaisha kuchukulia hatua za kinidhamu .

  Alisema kuna baadhi ya mahakimu vijijini wanatumika kunyanyasa wananchi kwa kupindisha sheria kusudi ili kujipatia fedha .

  "Kuna hakimu mmoja sitaki kumtaja jina ila yupo Halmashauri ya Iringa vijijini kwa kusudi anatumika kutoa hukumu kandamizi na kwa kushirikiana na mteja wake anashinikiza aliyeshinda kesi kufungua kesi ya madai ili fedha hizo wagawane......huu ni unyanyasaji mkubwa kwa kumpokonya haki mwenye haki ili kumpa asiye na haki"

  Hivyo alisema mafunzo hayo kwa madiwani na watendaji hao wa kata ni vema yakatumika kuwakomboa wananchi kwa kuwasaidia kujua sheria na kuwafichua wale wanaokiuka sheria na kuomba LASWA kuweka vijana wao waliopewa mafunzo ya kisheria kila ofisi ya mkuu wa wilaya ili kusaidia mambo ya kisheria badala ya kuwategemea wanasheria wa Halmashauri .

  Mkurugenzi wa LASWA Francis Mwilafi alisema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na asasi yake ya LASWA kwa ufadhili wa LSF ya jijini Dar es salaam kwa chini ya ubalozi wa Denmark kuwa sifa ya msaidizi wa kisheria ni kuwa na akili timamu pia sifa ya kuheshimu na kulinda sheria za mbali mbali za nchi na haki za binadamu

  Mkurugenzi huyo alisema hadi sasa wamekwisha toa mafunzo na kuwa na vijana katika wilaya zote tatu za mkoa wa Iringa ikiwemo ya Kilolo, Mufindi na Iringa kwa kuwa na vijana wasaidizi wa kisheria

  Aidha alisema faida kubwa ya msaidizi wa kisheria ni kupunguza na kuziba pengo la ukosefu wa huduma za msaada wa kisheria katika jamii anayoishi kwa kutoa usaidizi wa awali wa kisheria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DC KASESELA ASIFU KAZI ZA LASWA IRINGA,ATAKA MATAPELI WA MIKOPO YA RIBA KUBWA WAFICHULIWE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top