728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, October 18, 2016

  Dc Hapi aagiza Polisi kuvamia nyumba inayohifadhi wahalifu Magomeni

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi akizungumza na wakazi wa Magomeni Suna, Jijini Dar es Salaam leo, baada ya kusikiliza kero zao.

  Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii.

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi, amemwagiza Mkuu wa Polisi Kanda ya Magomeni Salum Morcase, kufanya uchunguzi wa kina katika nyumba zinazo sadikiwa kuwa zinahifadhi katika kata ya Magomeni Makuti.

  Hapi alitoa agizo hilo, baada ya kusikiliza kero ya wanachi wa kata ya Magomeni Suna, waliolalamika kuna nyumba inayotunza wahalifu imekuwa tishio katika mtaa wa Makuti.Hapi alimwagiza Mkuu wa Polisi kufanya doria katika eneo hilo, kwani nyumba hiyo imekuwa kero kwa wananchi.

  Mbali na kuwakamata wahalifu hao, Hapi aliagiza mmiliki wa nyumba hiyo kukamatwa ili aweze kuisaidia Polisi kukamatwan kwa wahalifu hao.Naye Mkazi wa eneo hilo Sabrina Ibrahimu alisema kuwa, nyumba hiyo inatunza vibaka, wavuta bangi, ambao wamekuwa kero kwa wananchi wa eneo hilo kwa kuwaibia fedha na mali zao.

  Ibrahim alisema kuwa, vijana wanaoishi katika nyumba hiyo wamekuwa wakivuta bangi nje ya adhara, huku wakiwahalaso hata watoto wa shule wanaopita nje yanyumba hiyo wakielekea shule.Aidha mkazi huyo alidai kuwa, nyumba hiyo imekuwa tishio katika maeneo hayo, huku Polis wakionekana kutochukua hatua yoyote licha ya kuwa jershi hilo linataarifa za uhalifu huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Dc Hapi aagiza Polisi kuvamia nyumba inayohifadhi wahalifu Magomeni Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top