728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, October 7, 2016

  DC CHEMBA AKEMEA NA KULAANI TABIA YA BAADHI YA WANANCHI KUJICHUKURIA SHERIA MKONONI

  Mkuu huyo wa Wilaya ya Chemba ameyasema hayo leo wakati wakiaga mwili wa Mke wa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kelema Balai aliyeuwa kwa kupigwa mshale wa sumu kijana ambaye mpaka sasa amekimbia na kutoweka hapo kijijini kutokana na ugomvi ambao umedumu kwa muda mrefu kati ya mume wa marehemu na kijana anayehisiwa kutenda unyama huu.

  Kijana anayehisiwa akiwa na wenzake wawili siku ya tukio majira ya saa mbili na nusu usiku walivamia nyumbani kwa marehemu na kuanza kumshambulia kwa fimbo mume wa marehemu na kukimbizwa hospital ya jirani kabla muhisiwa hajarejea na kutekeleza unyama huo.

  Mpaka sasa watu watatu wanashikiliwa na Polisi ambao ni baba wa kijana huyo kwa kuwa alishiriki katika tukio la awali la kumjeruhi Mwl Manyama kwa kushirikiana na kijana wake kumjeruhi kwa fimbo. (Mwl Manyama ndiye mume wa marehemu)

  Watu wengine ni Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na Mtendaji wa Kijiji. Hawa wanashikiliwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya baada ya maelezo yao waliyoyatoa kuhusiana na namna walivyoshughulikia tukio hili kuanzia usiku mpaka asubuhi kuto mridhisha Mkuu wa Wilaya. Kwani toka usiku wa tarehe 3 mpaka saa tatu wahisiwa walikuwepo kijijini kabla ya kutoweka na Viongozi hao hwakuwa wamechukua hatua zozote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DC CHEMBA AKEMEA NA KULAANI TABIA YA BAADHI YA WANANCHI KUJICHUKURIA SHERIA MKONONI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top