728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, October 17, 2016

  BALOZI WA TANZANIA NCHINI KOMORO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KOMORO, MHE. AZZALI OUSMAN

  Balozi Chabaka Kilumanga akipokea zawadi kutoka kwa Rais. Azzali Ousman
  Kutoka Kushoto Rais Azali Ousman, Balozi wat Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka Kilimunga, Bw. Mudrick Soragha Mkuu wa Afisa Ubalozi na Bi. Sheehat Kassim Mkalimani .
  Mhe. Chabaka Kilumanga Balozi wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Komoro leo tarehe 17 Oktoba, 2016 alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Col. Azzali Ousmani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Komoro katika Ikulu ya Bait Salam. Hii ni mara ya kwanza kwa Mhe. Rais Azzali kufanya mazungumzo na Balozi huyo kutoka Tanzania tangu kuingia kwake madarakani Tarehe 25 Mei, 2016. 

  Katika mazungumzo yao Mhe. Chabaka Kilumanga alichukua fursa hiyo kumpongeza Rais Azzali kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuongoza Wanakomoro na kuelezea kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wake kwa Komoro hasa kwa kuzingatia mahusiano yakaribu yaliyopo baina ya hizo mbili. 

  Kwa upande wake Mhe. Azzali Ousmani, Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Visiwa vya Komoro alimshukuru Mhe. Balozi kwa ushirikiano ambao amekuwa akiupata kutoka kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Komoro na kueleza kuwa Komoro inajifunza mambo mengi kutoka kwa ndugu zao wa Tanzania. 

  Aidha aliezea kuwa uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Komoro ni wa Kihistoria na ni matarajio yake kuwa uhasiano huo utaendelea kukuzwa na kudumishwa kwa manufaa ya nchi zote mbili. Wakati wakimaliza mazungumzo yao, Mhe. Azzali alieleza dhamira yake ya kutaka kufanya ziara nchini Tanzania na kwamba ni matarajio yake kuwa ziara hiyo itafanyika mapema iwezekanavyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BALOZI WA TANZANIA NCHINI KOMORO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KOMORO, MHE. AZZALI OUSMAN Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top