728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, October 9, 2016

  ALIEKUWA MWENYEKITI WA UWT DODOMA,MAREHEMU SALOME KIWAYA KUAGWA JIONI HII


  CCM Mkoa wa Dodoma pamoja na Jumuiya ya Wanawake Katoliki Tanzania (WAWATA) mkoa wa Dodoma muda huu wapo kwenye tukio la kutoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa  Salome Kiwaya aliyefarika juzi kwa ajali ya gari.

  Heshima hizo za mwisho zinatolewa mbele mwili huo uliowekwa ndani ya kanisa kuu la Jimbo Katoliki hapa mjin Dodoma.Marehemu Salome Kiwaya hadi mauti yake alikuwa M/k wa UWT mkoa pamoja na WAWATA Jimbo Kuu la Dodoma.

  Ibada ya misa kuuaga mwili huo, inategemewa kuanza saa 9:00 alasiri na baadae kusafirishwa kwenda Mkoa wa Njombe jioni hii, ambapo utazikwa huko kesho jumatatu.Hapa wapo viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali akiwamo RC Dodoma, Spika wa Bunge la Tanzania, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda na mkwe.

  Pia yupo M/k wa CCM mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa na wengine wengi.

  Kati ya hawa watatoa salamu za chama na serikali hapo baadae na watakachosema, nitakituma huko kwa ajili ya habari za kesho.

  Mungu ampumzishe kwa Amani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: ALIEKUWA MWENYEKITI WA UWT DODOMA,MAREHEMU SALOME KIWAYA KUAGWA JIONI HII Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top