728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, October 3, 2016

  Airtel Tanzania yazindua wiki ya huduma kwa wateja kwa kauli mbiu ya "Bingwa wa huduma"

  Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Airtel, Bi Adriana Lyamba akiongea wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa wateja ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ya Airtel ni Bingwa wa huduma .

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imezindua wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa  kila mwaka kwa lengo la kutambua umuhimu wa wateja wao na kuwapongeza watoa huduma wanaowahudumia wateja vizuri na kutatua mahitaji yao ya huduma za mawasiliano ya kila siku.

  Mwaka huu wiki ya huduma kwa wateja  itaanza leo jumatatu huku Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel Bi, Adriana Lyamba akisema “wiki ya huduma kwa wateja ni wiki muhimu sana kwa Airtel na ndio maana wamekuwa wakiiadhimisha kila mara kwa kuweka aina tofauti za matukio yanayolenga kuwaweka karibu sana na wateja kwa kuwahudumia vyema. "Mwaka huu tunatarajia kuendesha matukio tofauti wiki nzima kuanzia tarehe 3 -7 Oktoba 2016 ikiwa ni namna ya kuwashukuru wateja kwa kuendelea kutumia huduma zetu na kuwakaribisha wateja wengine wanaohamia  kwenye Familia ya Airtel" alisema Bi Lyamba.

  “Kaulimbiu ya Mwaka huu ni ‘Service Champions’ yaani ‘Bingwa wa Huduma’  tutaitimiza kwa kuhakikisha tunatoa suluhisho kwa mahitaji ya  wateja wetu sambamba na  kutoa huduma za viwango vya juu  zenye kuleta tija kwa jamii” Bi Lyamba alibainisha.

  Bi Lyamba aliendelea kusema.” Katika kusherehekea wiki hii na wateja wetu, Airtel tunajivunia kutoa huduma na bidhaa za kipekee na  kibunifu,   kupitia kampeni yetu ya “Sibanduki” tumewawezesha wateja zaidi ya million 10 kufaidika na huduma zetu na kuwapa sababu za kuendelea kutumia na kujiunga na  huduma zetu". 

  Huduma zetu za kipekee ikiwemo Vifurushi vya Yatosha, mikopo ya Timiza kwa wateja  na Mawakala,  kutuma pesa bure kwa kupitia Airtel Money, kufanya mihamala ya fedha yaani benki kwenda kwenye simu au kutoka kwenye simu kwenda banki yanaonyesha jinsi tulivyojikita katika kuhakikisha mteja anapata huduma za hali ya juu zinazokidhi mahitaji yake ya huduma za mawasiliano. Wateja wapya watakaojiunga na huduma zetu wiki hii kujiunga watapata dakika 160 za kupiga mitandao yote, sms 2000 na MB 200  Bure, kwa miezi miwili”

  “tunawakaribisha wateja kutembelea maduka yetu ya Airtel au smarphone Bazaar pale Mlimani City ili kuweza kujipatia simu za kisasa za Smartphone kwa gharama nafuu sana

  Airtel tumejipanga kuwahudumia kwa umakini ili kuweka kumbukumbu ya kwamba Airtel ni Bungwa wa kutoa huduma za Mawasiliano” alimaliza kwa kusema Bi Lyamba.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Airtel Tanzania yazindua wiki ya huduma kwa wateja kwa kauli mbiu ya "Bingwa wa huduma" Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top