728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 15, 2016

  Zaidi ya wafanyabiashara 100 wa Tanzania na Kongo kushiriki kongamano la Biashara

   Mratibu wa Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Congo DRC, Bi. Anna  Msonsa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Septemba 22 Jijini Lubumbashi, Congo. Kushoto ni Afisa Miradi wa Kampuni ya Uhusiano ya 361 Tanzania, Bi. Naomi Godwin.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Louis P. Accaro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Septemba 22 Jijini Lubumbashi, Congo. Kushoto ni Mratibu wa Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Congo DRC, Bi. Anna Msonsa.
  Meneja wa Masoko wa Kampuni ya GSM Group Bi. Farida Rubanza (kushoto) akielezea jambo wakati wa mkutanio wao na  waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Louis P. Accaro, Mratibu wa Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Congo DRC, Bi. Anna Msonsa na Afisa Miradi wa Kampuni ya Uhusiano ya 361 Tanzania, Bi. Naomi Godwin.Picha na Frank Shija, MAELEZO.

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO

  Zaidi ya wafanyabiashara 100 kutoka Tanzania na Kongo wanatarajia kushiriki kongamano la biashara litakalofanyika Lubumbashi Kongo Septemba 22 mwaka huu.

  Lengo la Kongamano hilo ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kuongeza kiasi cha mauzo ya nje na kuboreshwa mazingira mazuri ya biashara kati ya nchi hizo mbili.

  “Wafanyabiashara wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kupata soko nchini Kongo, kutokana na nchi hiyo kutegemea bidhaa nyingi kutoka Tanzania kama vile samaki wabichi na wakavu kutokana na nchi hiyo kutokuwa na bahari,” alifafanua Afisa biashara wa TANTRADE Bi. Getrude Ngwesheni.

  Aliendelea kwa kusema kuwa Kongo wanaongea lugha ya kiswahili kuwasiliana, lugha ambayo inatumika na watanzania wengi, hivyo itarahisisha mawasiliano katika shughuli za biashara.

  Kwa upande wake, Mratibu wa Kongamano hilo kutoka Chama cha wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bi. Anna Msonsa amesema kuwa kongamano hilo linatoa fursa kwa wafanyabiashara wote kuanzia wa chini mpaka wale wakubwa na kuwataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo.

  Akitoa maelezo ya namna ya kushiriki Kongamano hilo Afisa Miradi kutoka Kampuni ya 361 Bi. Naomi Godwin amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kujaza fomu ambazo zinapatika katika ofisi za 361 digrii zilizoko Msasani pamoja na ofisi za TCCIA na TANTRADE au kwa kutembelea tovuti ya www.tanzaniadrc.com.

  Aidha, kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Kongo, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Chama cha wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Shirikisho la wafanyabiashara wa Kongo (FEC), Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Taasisi ya Sekta Binafsi Nchi Tanzania (TPSF), Kampuni ya 361 Degrees na mdhamini mkuu ambaye ni Taasisi ya GSM Foundation.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Zaidi ya wafanyabiashara 100 wa Tanzania na Kongo kushiriki kongamano la Biashara Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top