728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 16, 2016

  WILDAF YAWASILISHA MAPENDEKEZO KUFUTA SHERIA ZA KIMILA ZINAZOSIMAMIA MIRATHI


  Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WILDAF) limewasilisha mapendekezo kwa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria likitaka kufutwa kwa sheria mbalimbali za kimila zinazosimamia masuala ya mirathi ambazo zinalalamikiwa kuwakandamiza wanawake nchini . 

  Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa WILDAF Bi. Judith Odunga amesema mapendekezo hayo yanataka kufutwa kwa sheria za kimila ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwakanadamiza wanawake na kuwanyima haki ya kumiliki mali na kufanyiwa vitendo vya kidhalilishaji pale wanapofiwa na waume zao. 

  Amesema katika mapendekezo hayo WILDAF inaiomba Serikali itunge sheria moja ambayo pamoja na zile za kidini itashughulikia masuala ya mirathi na kuweka usawa wa kisheria katika urithi wa mali kati ya mwanamke na mwanaume ikiwa ni pamoja na watoto wa kiume na wa kike kuwa na usawa katika kurithi mali inapotokea mzazi wa kiume amefariki. 

  “Tulipoonana na Mhe Waziri Dkt Mwakyembe alituagiza kama tunataka kuwasaidia wanawake nchini basi tuwasilishe wizarani mapendekezo yetu juu ya nini kifanyike, sasa leo tumekuja hapa kutekeleza agizo la Mhe Waziri, tunampatia Katibu Mkuu mapendekezo husika, ambayo kwa asilimia kubwa yanapendekeza kufutwa kwa sheria zote za kimila ambazo zinamkandamiza mwanamke na mtoto wa kike na kutungwa kwa Sheria moja itakayoshughulikia masuala yote ya mirathi nchini na tuna imani kuwa yatafanyiwa kazi na kufanikisha azma ya WILDAF ya kuwasaidia wanawake nchini, alisema Mwenyekiti wa WILDAF Bi. Judith Odunga 

  Akipokea mapendekezo hayo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijni Dar es Salaam amewapongeza na kuwashukuru WILDAF kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ili kuwasaidia wanawake na Serikali kwa ujumla wake kwani kitendo hicho kitasaidia sheria husika kufanyiwa marekebisho yatakayostahili ili ziendane na wakati, zikidhi mahitaji na kutafsiriwa katika lugha ambayo wananchi wengi ambao ndio walengwa wazielewe sheria hizo 

  Amesema sasa Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa sheria zote nchini zinatafsiriwa na zile zinazotungwa zitakuwa kwa Kiswahili na Kingereza, uamuazi ambao utawawezesha watanzania wengi kuzielewa sheria hizo. 

  Prof Mchome alaiwashukuru WILDAF kwa kazi waliyoifanya na kuwaadi kuwa wataalamu wake wizarani watayafanyia kazi mapendekezo yaoi ili kuhakikisha gurudumu la sheria nchini linasonga mbele na kuwasaidia wananchi wengi na kuwataka wadau wengine kuja wizarani kuzungumza pale watakapoona kuna haja ya kufanya hivyo kwani wizara ipo tayari kuwasilikiza na kuyafanyia kazi mapendekezo yao. 
  Mkurugenzi wa WILDAF Bi. Judith Odunga akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijni Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo hayo yanayotaka kufutwa kwa sheria za kimila nchini ambazo zinadaiwa kuwakandamiza wanawake kwa kuwanyima haki sawa ya kumiliki mali pindi wanapofiwa na waume au wazazi wao anaeshuhudia kushoto ni Bibi Thabita Siwale Mwenyekiti wa Kikosi cha kupambana na haki za mirathi Tanzania- KIKUHAMI.
  Wajumbe mbalimbali wa WILDAF walioambatana na Mwenyekiti kushuhudia uwasilishaji wa mapendekezo yao wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome Ofisini kwa jijini Dar es Salaam
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WILDAF YAWASILISHA MAPENDEKEZO KUFUTA SHERIA ZA KIMILA ZINAZOSIMAMIA MIRATHI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top