728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 23, 2016

  WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MAFIA, AIPA SIKU 10 TAASISI YA HIFADHI YA BAHARI KULIPA DENI LA SH. MILIONI 100

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa muda wa siku 10 kwa Taasisi ya Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu kulipa deni la sh. milioni 100 inayodaiwa na Halmashauri ya wilaya ya Mafia. 

  Deni hilo linatokana na malimbikizo ya miaka mitatu ya maduhuri yatokanayo na makusanyo yanayofanywa na taasisi hiyo katika maeneo ya hifadhi ya bahari wilayani humo.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 23, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo katika ukumbi Caltas akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi siku mbili. 

  “Waandikieni barua na muitume leo hii kwa njia ya mtandao (email) kuwajulisha kuwa wanatakiwa kulipa deni hilo ndani ya siku 10. Hakikisheni wanalipa deni hili ili Halmashauri iweze kufanya kazi zake vizuri,” amesema.
  Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona Halmashauri hiyo ikinufaika kutokana na vyanzo vyake vya mapato, hivyo haitakuwa tayari kuona ikihangaika.

  Mbali na agizo hilo, Waziri Mkuun amesema atafuatilia kuona wajibu wa taasisi hiyo na mipaka yao ikiwa ni pamoja na kujua mapato yatokanayo na shughuli hizo katika maeneo ya hifadhi.

  Awali mkuu wa wilaya ya Mafia Shaib Nnunduma alisema kuwa miongoni mwa changamoto zinazoikabili wilaya hiyo ni kutolipwa kwa wakati fedha za maduhuri yatokanayo na makusanyo yanayofanywa na Taasisi ya Hifadhi ya Bahari.

  Mkuu huyo wa wilaya ameiomba Serikali kuangalia upya majukumu ya taasisi hiyo na nafasi ya halmashauri katika kuendesha shughuli za uwekezaji pamoja na kupata mapato yatokanayo na shughuli hizo katika maeneo ya hifadhi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, SEPTEMBA 23, 2016.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kwa ziara ya kikazi wilayani humo Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  mafi2
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Pwani baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia  kwa ziara ya kikazi Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  maf3
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika sala ya Ijumaa kwenye Msikiti Mkuu wa Mafia akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Pwani Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  maf4
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka kwenye Msikiti Mkuu wa Mafia bbada ya kushiriki  sala ya Ijumaa akiwa katika siku ya kwanza na ziara  ya mkoa wa Pwani Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  maf5
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka kwenye Msikiti Mkuu wa Mafia bbada ya kushiriki  sala ya Ijumaa akiwa katika siku ya kwanza na ziara  ya mkoa wa Pwani Septemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MAFIA, AIPA SIKU 10 TAASISI YA HIFADHI YA BAHARI KULIPA DENI LA SH. MILIONI 100 Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top