728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, September 21, 2016

  WAVUVI KIJIJI CHA CHWAKA WAPIGA HATUA ,WADHIBITI UVUVI HARAMU  Na Fatma Makame MCC 21/09/2016.

  Wavuvi wa kijiji cha Chwaka wamepiga hatua ya kuweza kudhibiti uvuvi haramu kijijini humo kwa lengo la kuleta maendeleo ya uvuvi .

  Kauli hiyo imeetolewa na wananchi wa kijiji hicho wakati wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi, walisema kudhibitiwa kwa uvuvi haramu kijijini humo kumetokana na mashirikiano makubwa baina ya wananchi na wavuvi.

  Walisema mafanikio hayo yametokana na kuunda kwa kamati ya uvuvi yenye lengo la kuwasimamia shughuli zote za bahari pamoja na kufuata maelekezo yanayotolewa na Idara ya Uvuvi.

  “Kuundwa kwa kamati hiyo kumeweza kutatua matatizo mengi yanayotokana na uvuvi haramu na hasa pale yanapotokea maafa baharini,”walieleza

  Hata hivyo wameeleza kuwa Kamati hiyo imeweka mikakati kwa mvuvi yeyote atakae kwenda kinyume na taratibu ziliwekwa atachukuliwa hatua za kisheria.

  Aidha walifahamisha kuwa wavuvi wa kijiji hicho wanatarajia kupata msaada wa meli kupitia Idara ya uvuvi ambayo wataweza kuvua masafa ya mbali ili kuondokana na migongano na wavuvi wadogo wadogo .

  Nao Wavuvi hao walisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni uingiaji wa meli kutoka nje ya nchi kuja kuvua kijijini hapo jambo ambalo linapelekea kukosa mafanikio katika kazi yao hiyo na kurudi nyuma kimaisha.

  Pia wananchi hao wamewataka vijana kujishughulisha na kazi za kujipatia maendeleo ili kuepukana na vitendo viovu ambavyo havistahiki katika jamii .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAVUVI KIJIJI CHA CHWAKA WAPIGA HATUA ,WADHIBITI UVUVI HARAMU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top