728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, September 18, 2016

  Wateja wa Airtel wajipatia smartphone kwa bei ya bando

   
   Wateja wa Airtel wakijipatia simu za smartphone na kujiunga na team sibanduki katika smartphone bazaar iliyoko mlimani city, Smartphone Bazaar itakuwepo siku za mwisho wa wiki Jumamosi na  jumapili . simu za kijanja kama  Fero 280 na magnus z11 , Huawei Y3C na nyingine nyingi zinapatikana hapo.
   Muhudumu katika kitengo cha huduma kwa wateja akitoa elimu juu ya simu mbalimbali za kisasa kwa wateja waliotembelea Airtel Smartphone Bazaar , mlimani city

  Katika kuendeleza kampeni yake kabambe ya “Sibanduki”  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeweka gulio la simu yaani Smartphone Baazar  mwishoni mwa wiki ndani ya mlimani City jijini Dar es Saalam ili kuwawezesha wateja wake kupata simu za kisasa , origino na kwa gharama nafuu
  Airtel Smartphone Bazaar ina lengo la kuwapatia wateja wa Airtel simu za kisasa na pia kutoa nafasi kwa wateja wa Airtel kujiunga na timu Sibanduki” na kufurahia huduma lukuki ikiwemo ,kutuma na kutoa pesa bure, kujitengenezea vifurushi vya yatosha na kupata MB zaidi, SMS zaidi na intaneti zaidi,  kupata mikopo ya Timiza isiyo na dhamana, kutoa pesa benki na kuweka kwenye akaunti zao za Airtel Money wakati wowote na kwa wateja wapya kupata vifurushi vya dakika 60, SMS 2000 na MB 200 bure bila , vifurushi hivi vitadumu kwa muda wa siku 60
  Akiongea kuhusu Smartphone Bazaar, James Kagashe, Afisa bidhaa na masoko alisema “ Tunayofuraha kuwaletea sokoni wateja wetu simu za kisasa , origino na zenye gharama nafuu hadi shilingi 24,000. Tunazo simu nyingi ikiwemo simu Aina ya fero 280 inayouzwa 24,000, simu ya smartphone aina ya Magnus Z11 inayouzwa kwa shilingi 83,000 na simu ya Huawei Y3C kwa shilingi 140,000. Pamoja na simu hizi tunazo simu aina ya Samsung, Techno pia zinapatikana hapa katika Bazaar hii.
  Natoa wito kwa wateja na watanzania kujitokeza na kutembelea hapa ndani mlimani city na kujipatia simu kwa bei poa na kujiungana timu Sibanduki kwa huduma bora za kipekee na kibunifu wakati wote
  Smartphone Bazaar itakuwepo pia wiki ijayo siku ya Jumamosi na Jumapili hapo haop mlimani City

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Wateja wa Airtel wajipatia smartphone kwa bei ya bando Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top