728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 22, 2016

  WATALAAM WA TEHAMA WAPASWA KUTUMIA TEKNOLOJIA MPYA

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza wakati akifunga mkutano wa wadau wa sekta ya mawasiliano wa kujadili mkakati wa utekelezaji wa Sera mpya ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Mhandisi Clarence Ichwekeleza akitoa mada wakati wa Mkutano wa wadau wa sekta ya mawasiliano wa kujadili mkakati wa utekelezaji wa Sera mpya ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016
  Baadhi ya wadau wa sekta ya mawasiliano wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) akizungumza wakati akifunga mkutano wa wadau wa kujadili mkakati wa utekelezaji wa Sera mpya ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016

  ………………………………………………………………………….

  Na Ally Daud-Maelezo

  Wataalamu Wa tehama wamepaswa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa ya tehama ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo iliyopo kwa sasa ulimwenguni.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Faustin Kamuzora katika mkutano wa wadau wa tehama uliojadili utekelezaji wa mkakati wa Sera ya Tehama ya mwaka 2016

  Aliongeza kuwa wataalamu wa tehama wanapaswa kutumia njia mpya na za kisasa ili kukuza uchumi kama zinavyofanya nchi zilizoendelea duniani.

  “Wanatehama mnatakiwa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa ili kuweza kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati kwa kupitia teknolojia hiyo kama zifanyavyo nchi nyingine zilizoendelea duniani kote” alisema Prof. Kamuzora.

  Aidha Prof. Kamuzora alisema katika mkutano huo wanatarajia kupata mbinu mbadala za kupambana na uhalifu kwa kutumia mitandao katika kutekeleza mkakati wa Sera ya tehama ya mwaka 2016- 2020 ili kutekeleza mpango huo.

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza alisema kuwa moja ya mkakati wa mkutano huo ni kutengeneza miundombinu ya tehama kwa Watanzania waweze kufikiwa kirahisi.

  Aidha mhandisi Ichwekeleza alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2018 inaandaa mkakati maalum wa kuwalinda watoto kutokana na madhara ya Tehama ili kuweza kuwasaidia watoto kukua katika misingi bora inayoendana na jamii ya Tanzania.

  Mkutano huo uliwakutanisha wadau mbalimbali Wa mitandao ya simu pamoja na wataalamu Wa tehama nchini ili kujadili mkakati wa Sera ya Tehama ya mwaka 2016.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WATALAAM WA TEHAMA WAPASWA KUTUMIA TEKNOLOJIA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top