728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 8, 2016

  WASHRIKI MISS KINONDONI WAPIGA JEKI UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA WILAYANI KINONDONI

   
   Picha ya Pamoja
   Miss kinondoni 2016 pamoja na washiriki wengine wakikabidhi asilimia 10% ya mapato kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa  kwa mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh.Hapi ambayo yalipatikana katika hafla fupi ya kumpata mwakilishi wa miss kinondoni 2016  WAREMBO walioshiriki shindano la Miss Kinondoni 2016, wamekabidhi msaada wa fedha taslimu Sh. milioni moja kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa ya shule zilizopo katika wilaya hiyo.

  Wakikabidhi fedha hizo jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi walipomtembelea ofisi kwake, mshindi wa shindano hilo, Diana Edward, alisema kuwa wamefanya hivyo wakitimiza ahadi yao waliyoitoa walipomtembelea kiongozi huyo mwezi uliopita.

  “Tulipokuja ofisi kwako, tuliahidi kutoa asilimia 10 ya mapato ya viingilio kusaidia ujenzi wa madarasa na leo tumekuja kutimiza ahadi yetu ili kuwasaidia wadogo zetu waweze kupata elimu katika mazingira bora yatakayowawezesha kuelewa vizuri zaidi masomo yao,” alisema.

  Akipokea msaada huo, Hapi aliwashuku warembo hao na kamati ya Miss Kinondoni kwa ujumla kwa kuonyesha kuguswa na jitihada za Rais John Magufuli za kuboresha elimu nchini, akitoa wito kwa wadau wengine kumuunga mkono kiongozi huyo wa nchi.

  Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mh. Hapi, msemaji wa Rahmat Entertainmen, waandaaji wa Miss Kinondoni, George Yusuph, alimtaka mkuu huyo wa wilaya kuendelea kuwasapoti katika mashindano ya mwakani, huku akitamba taji la Miss Tanzania mwaka huu kutua Kinondoni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WASHRIKI MISS KINONDONI WAPIGA JEKI UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA WILAYANI KINONDONI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top