728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, September 21, 2016

  WANANCHI KIJIJI CHA DUNGA KIEMBENI WALIOMBA JESHI LA POLISI KUFUATILIA TATIZO LA WIZI WA MIFUGO


  Na Fatma Makame MCC 21/9/2016

  Wananchi wa kijiji cha Dunga kiembeni wameliomba Jeshi la Polisi kufuatilia tatizo la wizi wa mifugo jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo .

  Akizungumza na waandishi wa habari hizi Ali Juma Salum amesema tatizo hilo limekithiri kijijini hapo kwani hupelekea wafugaji kuvunjika moyo kutokana na kupungua idadi ya mifugo yao .

  Alisema wizi huo unatokana na vijana wengi kutojishughulisha na kazi za mikono za kujipatia kipato cha kuweza kijikimu kimaisha jambo ambalo linachangia kuzorotesha maendeleo .

  “Vijana wanapenda kutumia bila kujishughulisha na kazi yeyote hatimae kujiingiza katika vitendo vya wizi wa mifugo”alisema Ali Juma.

  Aidha alisema wafugaji wengi wanakata tamaa kutokana na wizi wa mifugo mbali mbali ikiwemo n’gombe, mbuzi ,kuku, pamoja na bata jambo ambalo linawatia hasara katika ufugaji wao .

  Nae Mjumbe wa Sheha wa Shehia hiyo Kesi Makame Mussa amekiri kuwepo kwa vitendo hivyo na kuwataka wananchi waendelee na ufugaji na tatizo hilo litatafutiwa ufumbuzi .

  Hata hivyo sheha huyo amesema atahakikisha anashirikiana na Jeshi la Polisi ili kupunguza vitendo hivyo katika kijiji hicho.

  Sambamba na hayo amewata wananchi wawe na mashirikiano ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa . 

  MWISHO IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WANANCHI KIJIJI CHA DUNGA KIEMBENI WALIOMBA JESHI LA POLISI KUFUATILIA TATIZO LA WIZI WA MIFUGO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top