728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, September 7, 2016

  Wananchi Babati wazinduliwa mradi wa maji na mwenge wa uhuru


  Mkimbiza mwenge kitaifa Lucia Kamafa akimtwisha ndoo ya maji Mariam Mollel mkazi wa Gunge Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambpo ukiwa Mkoani humo ulitembelea miradi yenye thamani ya sh7.7 bilioni.

  Mwenge wa uhuru ukikimbizwa kwenye Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambapo ulizindua miradi yenye thamani ya zaidi ya sh1 bilioni.


  Wakazi 2,986 wa Kijiji cha Endanachan Wilayani Babati Mkoani Manyara, waliokuwa wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji, wameondokana na changamoto hiyo baada ya kuzinduliwa mradi wao utakaozalisha lita 144,000 kwa siku.

  Akizindua mradi huo, kiongozi wa mbio za mwenge uhuru kitaifa George Mbijima aliwataka wakazi hao kuuchunga na kuutunza mradi huo kwani serikali imetumia gharama kubwa hadi kufanikisha kuwapatia maji wananchi wake.

  Mbijima alisema maji ni hitaji kubwa la jamii hivyo itakuwa jambo la ajabu endapo baada ya muda mfupi, miundombinu ya mradi huo ukaharibika kwani haitakuwa sifa nzuri kwa jamii kususiana na tukio hilo.

  Ofisa mtendaji wa kijiji cha Endanachan Amos Gurti alisema mradi hadi kukamilika mradi huo umegharimu sh286 milioni, ikiwemo sh29 milioni za wananchi, sh600 milioni za halmashauri na sh256 milioni za wahisani wa Water aid na Kanisa katoliki jimbo la Mbulu, (DMDD).

  Alisema kupitia mradi huo wananchi wengi zaidi watapata huduma bora kwani una vituo tisa vya kuchotea maji ya bomba, bomba za usafirishaji kilometa 1.2 bomba za usambazaji kilometa 7.1 na tenki moja lenge ujazo wa lita 50.

  “Usimamizi na uendeshaji wa mradi huu unategemea zaidi mapato yanayotokana na ankara za maji yanayochotwa na wananchi wa hapa ambapo ndoo moja ya maji yenye ujazo wa lita 20 huuzwa kwa sh25,” alisema Gurti.

  Mmoja kati ya wakazi hao Martha Lowri alisema awali walikuwa wanatembea umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma ya maji ila baada ya huduma hiyo kuanzishwa watakuwa wamerahisishiwa kazi ya kufuata maji mbali.

  Lowri alisema hivi sasa hata mahusiano yao ya ndoa kwenye nyumba za wanawake wa eneo hilo utakuwa mzuri kwani hawatatembea tena umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma hiyo mbali na majumbani mwao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Wananchi Babati wazinduliwa mradi wa maji na mwenge wa uhuru Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top