728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, September 24, 2016

  WAFANYA BIASHARA KARIAKOO WACHANGIA MILIONI 60 WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA  NA HERIETH SEMGAZA


  Wafanyabiashara katika soko la kariakoo lililopo jijini Dares salaam wameombwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kuwachangia wahanga wa tetemeko la Bukoba mkoani Kagera leo katika harambee iliyofanyika katikati ya soko la Kariakoo jijini Dar es salaam

  Hayo yamesemwa na Philimin Romano Chonde Mwenyekiti wa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo(JWK) ambapo alitaja jumla ya pesa na thamani ya vifaa mbalimbali vilivyochangwa katika kampeni ya hiyo ,ambayo bado inaendelea amesema mpaka sasa wamepokea Jumla ya shilingi milioni 60 laki saba na mia Tano zimekusanywa  Philimin Romano Chonde amesema tunaendelea kupokea mchango wenu ili tuweze kuwasilisha kwa Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa katika siku itakayopangwa, Aidha amewapongeza wanachama,wafanyabiashara wote waliojitokeza kutoa michango yao na kuwataka waendelee kujitoa katika shughuri mbalimbali za Kitaifa.

  Nae SILVER MANDE mhazini Wa JWK amesema kuwa taasisi na wafanyabiashara wengine waendelee kujitokeza kwa wingi ili kutoa michango yao na kufanikisha kazi hiyo ambayo ni muhimu sana katika jamii yetu hasa kwa hawa wenzetu ambao walipata jamnga la Tetemeko la Ardhi huko Bukoba na kuathiri maisha yao na shughuli zao za kila siku.
  Taasisi mbalimbali na wafanyabiashara tunaomba muwe mstari wa mbele kutoa michango na kwa yeyote atakaye kuwanacho alete ili tuweze kujumuisha rambirambi zetu na kuwasilisha kwa Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAFANYA BIASHARA KARIAKOO WACHANGIA MILIONI 60 WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top