728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 15, 2016

  Vodacom yachangisha msaada wa wahanga wa tetemeko la ardhi.

  Mkuu wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza,akionesha namba maalumu 155990 ya kupokea msaada wa fedha kupitia huduma ya M PESA ambapo watanzania wote wanaombwa kuchangia wahanga wa tetemeko lililotokea mkoani Kagera hivi karibuni.

  ·         Ni kutumia namba maalum ya  kusaidia wakati wa majanga 155990.
  KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeeleza kuguswa na tukio la tetemeko la ardhi mkoani Kagera ambalo limesababisha vifo vya watu 16 na wengine mamia kujeruhiwa na kuacha familia nyingi zikiwa hazina makazi na kuanzia leo imeanza kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tukio hilo kupitia mtandao wake wa simu.

  Akiongea na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza amesema anawaomba watanzania wote wanaotaka kuchangia wahanga hao kutuma fedha zao kwenye namba maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya 155990.

  “Tukiwa kama kampuni ya mawasiliano tumeguswa na tukio hili na tunawapa pole waathirika wote na kuungana na wakazi wa Kagera kwa janga hili na tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kupitia taasisi yetu ya kusaidia jamii ya Vodacom Tanzania Foundation tunawaomba watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao na tutahakikisha tunaifikisha sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu ambao wako katika mazingira magumu na wanahitaji msaada wa haraka”.

  Alisema kupitia njia hii ya namba maalumu ya ”Vodacom Foundation Red Alert” 155990 ya kuchangisha fedha imewahi kurahishisha uchangishaji wa fedha kwa waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na kuathiri wananchi moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto jijini Dar es Salaam na aliwahimiza wananchi kuitumia kama njia rahisi ya uchangiaji. Mwisho wa uchangiaji ni tarehe 24 Septemba 2016, na vitu yatanunuliwa kutokana na uhitaji wa wakati huo.

   Jinsi ya kuchangia ni rahisi sana unachotakiwa kufanya unabonyeza *150*00#kisha aunachagua namba 4 yaani Lipa kwa M-PESA baada ya hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba 155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Vodacom yachangisha msaada wa wahanga wa tetemeko la ardhi. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top