728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, September 26, 2016

  Vodacom kuendeleza kuunga mkono kampeniza Usalama Barabarani.


   Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani, Mheshimi wa Hamad Masauni amesema kuwa bado kuna matukio mengi ya ajali za barabarani nchini zinaso sababisha vifo vya wananchi wengi hivyo kuna haja ya kuongeza nguvu katika kampeni za Usalama barabarani ili kupunguza tatizohili.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni (wapilikulia), akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango mkubwa wa  wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia), wakati wa uzinduzi wahafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanjawa Kalangala la mkoani Geita, na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Geita Ezekiel Kyunga (kushoto) na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Kamanda Mohamed Mpinga.Wasanii wa maigizo wa Futuhi wa kitumbuiza kwenye viwanjawa Kalangalala mkoani Geita, wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania, yenye kauli mbiu” Hatuta kiajali,tunataka kuishi”.
  NAIBUWaziri Masauni aliyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika kitaifa mkoani Geita ambapo pia alitumia fursahiyo kuyapongeza makampuni ya kibiashara na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayosaidiana na serikali kupitia Jeshi la Polisi kufadhili na kuendesha kampeni za Usalama barabarani.
  “Pamoja na kuwepo na matukio mengi ya ajali serikali inafarijika kuona yapo makampuni ya kibiashara na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanashirikiana kwa karibu na serikali kupitia Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani kuendesha kampeni za Usalama barabarani kwa jamiii kiwemo kufadhili shughuli za uhamasishaji Usalama katika Wiki hii ya Nenda kwa Usalama barabarani”.Alisema Mh.Masauni.
  Aliongeza kuwa jukumu hili  la kutoa elimu ya Usalama barabarani sio la Jeshi la polisi pekee bali kunahitajika ushirikiano kutoka  kwa wananchi wote kwa kuwa kila mmoja ni mtumiaji wa barabara na vyombo vya usafiri na aliwataka madereva kuzingatia sheria na kanuni za Usalama barabarani.
  Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha kampeni za Usalama barabarani kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Usalama barabarani na Kikosi cha jeshi la  polisi cha Usalama barabarani.
  Katika miaka mitatu mfululizo Vodacom imekuwa ikifadhili Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani ambapo mwaka huu imetumia zaidi ya shilingi milioni 48 kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza matukio ya ajali nchini katika uhamasishaji wa usalama katika kipindi hiki. 
  pia imekuwa ikiendesha kampeni za usalama kwa madereva na makundi mbalimbali ya jamii kwa kushirikiana na wadau wengine wa masuala ya  usalama barabarani. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia,amesema kuwa Vodacom itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza matukio ya ajali nchini. 
  “Kama Kampuni ya mawasiliano tumekuwa tukiendesha kampeni inayojulikana kama ‘Wait to Send’ ambayo imekuwa ikihamasisha madereva kutotumia simu za mkononi wakati wanaendesha vyombo vya moto ikiwemo kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wametumia vinywaji vyenye kilevi”.Alisema Mworia.
  Mworia pia alisema kuwa kampuni imekuja na mkakati wa kuhakikisha elimu ya usalama barabarani inawafikia wanafunzi wa shule za msingi ili wawe wakiwa na uelewa wa umuhimu wa kuzingatia kanuni za usalama barabarani ambapo kwa kushirikianana Jeshi la Polisi imekuwa ikiendesha mafunzo kwa wanafunzi wa shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Vodacom kuendeleza kuunga mkono kampeniza Usalama Barabarani. Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top