728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 15, 2016

  VISIMA 7 KUPUNGUZA TATIZO LA MAJI KISHAPU

  Youth Climate Activist Network (YouthCAN) Tanzania Ni mtandao wa vijana wanaotoka kwenye taasisi za dini mbalimbali wanaofanya shuguli mbalimbali za mazingira na afya kwa ujumla kwa kujitolea chini ya Shirika la Norwegian Church Aid (NCA)

  Kuanzia Tarehe 11/9 /2016 vijana hawa walianza masafara wa Kutembelea baadhi ya maeneo yaliyo athirika sana na mabadiliko ya tabia nchi. Ili kutoa elimu ya Utunzaji wa mazingira, vyanzo vya maji na usafi .baada ya kutoa elimu hiyo Halmashauri ya wiliya Kishapu Mkoani Shinyanga wanatarajia kwenda Kutoa elimu hiyo Mkoani Manyara kwenye baadhi ya vijiji vilivyopo Hanang.Hydom na Mbulu.

  Licha ya kutoa elimu juu mazingira,Maji ana afya vijana hawa watapata nafasi ya kuzindua baadhi ya Visima vya maji vilivyo jengwa na Shirika la Norwegian Church Aid (NCA) kwa kushirikiana na Washirika wake.

  Ambapo kwa kuanza wamepata fursa ya kushiriki uzinduzi wa visima 7 vilivyojengwa kwa msaada wa watu wa Norway visima hivyo vitasaidia kutatua tatizo la maji safi na salama katika vijiji vi 3 wiliyani Kishapu .ambavyo ni IKONDA A,UBATA na MWAWEJI.

  Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya Kishapu Bwana.Stephen M Magoiga akizindua moja kati ya Visima saba.

  Afisa Mradi Mwandamizi Mama Tina Mosha Akimtwisha maji Moja ya wanakiji wa IKONDA.
  Nizar Selemani Mratibu wa shuguli za vijana katika shirika la NCA na Baraka Chedego ambae ni Mratibu wa Youth CAN wakizungumza jambo wakati wa mkutano na wanakijiji cha Ikonda.
  Moja visima vilivyokuwa vikitumiwa na wanachi kabla ya ujenzi wa visima vya kisasa.
  Vijana wa YouthCAN wakitoa elimu ya Mazingira,Maji na Afya kwa njia ya Nyimbo Kijijini Ikonda.
  ikundi Mvalimbali vya sanaa kutoka Kishapu vikitoa burudani wakati wa Mkutano.
  Wananchi wa Kishapu wakifatilia mkutano kwa Umakini Mkubwa.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: VISIMA 7 KUPUNGUZA TATIZO LA MAJI KISHAPU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top