728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, September 24, 2016

  VIJIJI 24 WILAYANI KASULU KUPATA UMEME WA REA AWAMU YA PILI HADI MWISHONI MWA OCTOBA 2016.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wapili kulia) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe wilayani Kasulu. Kulia ni Mbunge wa Kasulu, Daniel Nsanzugwanko na kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wananchi wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo
  Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi. 
  *************
  WANANCHI wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, wanataraji kuanza kufaidi umeme wa REA pindi awamu ya pili ya mradi huo itakapo kamilika mwishoni mwa  Octoba 2016.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, alipotembelea miundombinu ya Umeme wa REA katika Wilaya ya Kasulu.

  Waziri Muhongo yupo katika ziara ya siku tano mkoani Kigoma kuangalia utekelezaji wa awamu ya pili ya miradi ya REA mkoani humo na Wilayani Kasulu aliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Martin Mkisi.

  Prof Muhongo, akiambatana na Wahandisi wa Tanesco, REA na Wakandarasi wanaojenga miundombinu hiyo, wamezungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe na Heru Juu Wilayani Kasulu.

   Aidha katika awamu ya tatu, vijiji vipatavyo 29 vitakamilishiwa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya umeme, kuchangamkia fursa za kufunga umeme wa bei rahisi na kujitokeza kwa wingi kwenye  mafunzo yatakayotolewa na Tanesco kuhusu umeme wa REA.

  Pia amewaagiza wakandarasi kukamilisha usambazaji wa huduma hiyo ifikapo Octoba 30 mwaka huu bila kuongeza siku hata moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: VIJIJI 24 WILAYANI KASULU KUPATA UMEME WA REA AWAMU YA PILI HADI MWISHONI MWA OCTOBA 2016. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top