728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, September 15, 2016

  UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA KWA WAHESHIMIWA WABUNGE -DODOMA

  Mbunge wa Muheza na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Bunge Mheshimiwa Adadi Rajabu akipokea kitambulisho chake kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati NIDA Bi. Rose Mdami katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.

  Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa jimbo la Musoma, Mhe.Profesa Sospeter Muhongo akipokea Kitembulisho chake cha Taifa chenye saini kwa furaha kubwa kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Na Hifadhi Hati NIDA. Bi. Rose Mdami
  Mheshimiwa Waziri wa Katiba na na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe, akiwa mwenye furaha kubwa baada ya kuchukua Kitambulisho chake kipya Bungeni Dodoma. NIDA imeanza kutoa vitambulisho vipya vyenye saini kwa viongozi wakiwemo Waheshimiwa Wabunge zoezi linaloedelea mkoani Dodoma sambamba na kikao cha Bunge
  Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mheshimiwa Andrew Chenge akisilikiliza kwa makini maelezo kuhusu Kitambulisho Kipya cha Taifa kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati NIDA Bi. Rose Mdami Bungeni Dodoma alipofika kuchukua kitambulisho chake mapema leo
  Mbunge wa Vita Maalum Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Dr. Elly Macha akipokea kwa furaha Kitambulisho chake kipya chenye saini kutoka kwa Afisa Usajili Wilaya ya Dodoma Mjini Bwana Khalid Mrisho
  Mheshimiwa Deo Sanga, akieleza faida ambazo tayari ameshazipata kwa kutumia Kitambulisho chake cha Taifa. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi hati NIDA Bi, Rose Mdami. Mhe. Sanga amepokea kitambulisho chake leo katika Ofisi za Bunge Dodoma
  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipata huduma kutoka kwa maafisa wa NIDA ambao wapo bungeni hapo kutoa vitambulisho vipya kwa waheshimiwa wabunge Mjini Dodoma
  …………………………………………………………………….

  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameendelea kuwa miongoni mwa wananchi walioanza kuchukua Vitambulisho vipya vya Taifa vyenye saini; kufuatia utaratibu uliotangazwa hivi karibuni na Nida wa kuanza kugawa vitambulisho vipya kwa makundi mbalimbali waliokamilisha taratibu za usajili

  Shughuli ya kugawa Vitambulisho vya Taifa kwa Waheshimiwa Wabunge zimeendelea katika siku ya pili bungeni Dodoma; pamoja na kuwasajili wabunge ambao kwa sababu moja au nyingine hawakusajiliwa wakati wa zoezi la awali la usajili

  Mbali na waheshimiwa Wabunge; wengine ni wafanyakazi wa Bunge na watumishi katika taasisi na Wizara mbalimbali ambao walisajiliwa katika utaratibu wa kawaida wa Usajili. Zaidi ya waheshimiwa Wabunge 240 watapatiwa vitambulisho vyao

  Zoezi la ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa linaendelea katika ofisi zote za usajili za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwa wale wananchi ambao hawakuwahi kupata vitambulisho awali. Kwasasa hakutakuwa na kubadilisha vitambulisho vya zamani kwa wale waliokwisha pata awali kwani Vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika sambamba na vipya katika matumizi mbalimbali yaliyokusudiwa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA KWA WAHESHIMIWA WABUNGE -DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top