728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, September 23, 2016

  Tume ya Mipango yatoa Elimu juu ya Mipango ya Maendeleo ya Kimataifa na Kikanda

                         
  Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe  (kushoto) akiongea na wadau wa sera na Mipango kutoka tasisi mbalimbali juu ya mikakati na mipango ya maendeleo ya Kimataifa na Kikanda. Katikati ni Balozi Innocent Shiyo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na kulia ni Bw. Maxwell Mkumba kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
  Wadau wa sera na mipango wakisikiliza moja ya mada zilizotolewa katika warsha hiyo.
                    Washiriki wakiwa wanasikiliza mada juu ya Mpango wa maendeleo wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).         

  Na Adili Mhina.
  Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa pamoja na Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) imeendesha warsha ya kujenga uelewa juu ya Dira na mipango ya maendeleo ya  kimataifa na kikanda.

  Warsha hiyo imewakutanaisha wakurugenzi wa mipango na sera kutoka sekta mbalimbali, idara na mashirika ya Umma, wawakilishi wa asasi zisizo za kiraia, wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na wataalam kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

  Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Paul Sangawe alisema warsha hiyo imekusudiwa kujenga uelewa juu ya Sera, mikakati na mipango ya maendeleo ya kimataifa na kikanda hususani malengo ya maendeleo endelevu 2030, Agenda ya maendeleo ya Afrika 2063, na mpango mkakati wa nchi za kusini mwa Afrika 2016/17-2010/21.

  Alieleza kuwa walengwa katika warsha hiyo watapata uelewa juu ya kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa sera, mikakati na mipango ya maendeleo ya kimataifa na kikanda.

  Warsha hiyo inayoendelea katika ukumbi wa kituo cha mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam itasaidia wadau kupata uzoefu kutoka nchi zingine wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Tume ya Mipango yatoa Elimu juu ya Mipango ya Maendeleo ya Kimataifa na Kikanda Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top