728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, September 26, 2016

  TRA YA WAHAMASISHA WAUMINI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA KUJENGA UTAMADUNI WA KULIPA KODI NA KUDAI RISITI.
  Afisa Mwandamizi Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi.Rose Mahendeka akizungumza na waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti wakati wa manunuzi ili kodi hii isaidie kuendesha shughuli za serikali katika kutoa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na afya,elimu,maji,miundombinu,ulinzi na usalama.
  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akisoma jarida lenye maelezo na taarifa za ulipaji wa kodi lilitolewa na mamlaka ya mapato Tanzania wakati wa semina iliyokuwa ikitolewa na maofisa wa mamlaka ya mapato Tanzania kwa waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Ndugu Amon Mpanju na kushoto kwake ni mkewe Grace Gwajima.
  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwasisitiza wauminiwake kulipa kodi ili kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
  Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (mstari wa mbele) wakiwa tayari kutoa mada ya uhamasishaji wa ulipaji kodi na umuhimu wa kudai risiti kwa waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima.
  Naibu Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Ndugu Amon Mpanju akizungumza na waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na umuhimu wa waumini hao kujua wajibu wao kwenye kulipa kodi.


  Na Frank Shija ,MAELEZO

  WATANZANIA wameaswa kujenga utamaduni wa kulipa kodi na kudai risiti pindi wanapofanya biasha au kununua bidhaa ili kuisaidia Serikali kukusanya mapato kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za kijamii.

  Wito huo umetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bibi. Rose Mahendeka alipokuwa akitoa elimu kwa waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.

  Rose alisema kuwa shughuli za Serikali katika nchi yeyote duniani, ikiwemo Tanzania zinagharamiwa na fedha zinazotokana na kodi pamoja na tozo mbalimbali.

  “Katika maandiko matakatifu imeandikwa; Ya Kaisari mpeni Kaisari, vya Mungu mpeni Mungu, hivyo ni vyema tukajenga utamaduni wa kulipa kodi na kudai risiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu”. Alisema Rose.

  Alisema umuhimu wa kudai risiti kuwa ni pamoja mwananchi kutambua kiasi cha kodi anayochangia Serikali yake, kutambua kodi halisi inayotakiwa kulipwa na ushahidi wa ununuzi wa bidhaa na uhalali wa umiliki wake.

  Aliongeza kuwa kutodai risiti ni kwenda kinyume na matakwa ya sheria ya mlipa kodi ambapo adhabu yake ni faini ya pointi za fedha 2 hadi 100 ambazo ni sawa na shilingi 30,000 mpaka 1,500,000/=.

  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Amon Mpanju aliupongeza uongozi wa Kanisa hilo kwa kuona haja ya waumini wake kupatiwa elimu ya mlipa kodi. Aidha aliwaka waumini wa kanisa hilo kulipa kodi na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya kuwa na Tanzania mpya kama ambavyo baba wa Kanisa hilo Askofu Josephat Gwajima amekuwa akisisitiza.

  Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima amewahimiza waumini wake kuishika na kuitumia elimu waliyopata kutoka kwa mwakilishi wa TRA ambapo aliwataka waumini hao kujenga utamaduni wa kudai risiti kila anapofanya malipo ili kusaidia ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TRA YA WAHAMASISHA WAUMINI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA KUJENGA UTAMADUNI WA KULIPA KODI NA KUDAI RISITI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top