728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, September 10, 2016

  Tetemeko Ardhi lenye Nguvu ya 5.7 lazua taharuki mkoani Kagera,labomoa nyumba na kujeruhi

  Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanywa mahali pamoja kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuathiriwa na taharuki hiyo kufuatia tetemeko la ardhi kutokea mkoani humo

   
   

  Nyumba kadhaa Mkoani Kagera zimebomoka baada ya tetemeko la Ardhi lenye nguvu ya 5.7 kipimo cha Ritcher kupita kwenye mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa.

  Taarifa zinadai Mji wa Kamachumu Mkoani Kagera ndio umeathiriwa Vibaya na tetemeko hilo, ambapo nyumba nyingi zimebomolewa.

  Hadi sasa hakuna idadi ya vifo au Majeruhi iliyotolewa na Mamlaka zinazohusika mkoani Kagera.

  Globu ya Jamii bado inaendelea kufuatilia kwa ukaribu taarifa za tukio hilo.


  Gari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mjini Bukoba likiwa katika harakati za Uokoaji.

  Nyumba Moja wapo ambayo imeathirika na Tetemeko hilo lililotokea Muda mfupi uliopita Mjini Bukoba.

  Nyumba ikionekana kupata nyufa baada ya tetemeko la Ardhi kuutikisa Mji wa Bukoba hivi Punde

  Milango ya Geti katika nyumba hiyo ikionekana kuanguka chini baada ya kukumbwa na dhoruba ya tetemeko la Ardhi, lililotikisa Mji wa Bukoba.
  Baadhi ya Nyumba za Wananchi wa Mji wa Bukoba Zikiwa katika hali Mbaya baada ya Tetemeko la Ardhi Kupita. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Tetemeko Ardhi lenye Nguvu ya 5.7 lazua taharuki mkoani Kagera,labomoa nyumba na kujeruhi Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top