728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, September 6, 2016

  TANZANITEONE YAJIPANGA KUENDELEA KUDHAMINI MICHEZO

  Kampuni ya TanzaniteOne ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kuunga mkono michezo mbalimbali ili kuhakikisha wanamichezo wanapiga hatua.

  Ofisa mahusiano wa kampuni hiyo Halfan Hayesh alisema japokuwa TanzaniteOne imedhamini michezo mingi hadi sasa, itaendelea kujitolea mara kwa mara kuwasaidia wanamichezo.

  Alisema hivi karibuni walimdhamini mwanamichezo wa mbio za magari na pia wakazifadhili timu nne za soka za mkoa wa Manyara, kwa kuzipatia vifaa vya michezo ikiwemo suti na sare za michezo, mipira, na sare za waamuzi.

  “Tunawaahidi wapenzi wa michezo kuwa tutaendelea kuwadhamini wanamichezo kwani hivi karibuni tulidhamini gari moja kwenye mbio za magari na kuwakilishwa na dereva Shanbhai na msaidizi Mwangi,” alisema Hayesh.

  Alisema pia walishadhamini michezo mingine ya burudani ikiwemo ya miss kanda ya kaskazini, miss Arusha, Miss Manyara na Miss Mirerani na wataendelea na udhamini wa michezo tofauti ili kusaidia maeneo yote.

  Alisema anatambua kupitia michezo kuna vipaji vingi vitagunduliwa hivyo kampuni hiyo itaendelea kuthamini suala hilo kwani michezo ni ajira, afya, upendeo, furaha, burudani na kujenga mshikamano na jamii inayowazunguka
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TANZANITEONE YAJIPANGA KUENDELEA KUDHAMINI MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top